Matendo 11
11
1BASSI mitume na ndugu waliokuwa katika Yahudi wakapata khabari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Bwana. 2Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakashindana nae, wakisema, 3Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. 4Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema, 5Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia. 6Nikaitazama sana, nikifikiri, nikaona nyama za inchi zenye miguu mine, Ua nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga. 7Nikasikia sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. 8Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najis hakijaingia kinywani mwangu. 9Sauti ikanijibu marra ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najis. 10Jambo hili likatendeka marra tatu, kiisha vitu vyote vikavutwa juu tena mbinguni. 11Kumbe! marra hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba niliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria. 12Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule: 13akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yoppa ukamwite Simon, aitwae Petro 14atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote. 15Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukia kama alivyotushukia sisi mwanzo. 16Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu. 17Bassi ikiwa Mwenyiezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu? 18Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.
19Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao. 20Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu. 21Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana. 22Khabari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wakaintuma Barnaba, aende hatta Antiokia. 23Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo. 24Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana. 25Barnabi tikatoka akaenda Tarso kumtafuta Saul: hatta alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. 26Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia. 27Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia. 28Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari. 29Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi. 30Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 11: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: