Matendo 15
15
1WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka. 2Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo. 3Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. 4Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. 5Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.
6Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo. 7Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. 8Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi; 9wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. 10Bassi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka nira juu ya shingo za wanafunzi, ambayo baba zetu na sisi hatukuweza kuichukua. 11Bali twaamini kwamba kwa neema ya Bwana Yesu tutaokoka kama wao.
12Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.
13Na bao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akinena, Ndugu zangu, nisikilizeni, 14Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. 15Na maneno ya manabii yapatana na bayo, kama ilivyoandikwa:
16Baada ya mambo haya nitarejea,
Nami nitaijenga tena nyumba ya Daud iliyoanguka.
Nitajenga tena maanguko yake,
Na nitaisimamisha;
17Illi wana Adamu waliosalia wamtafute Bwana,
Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao:
Asema Bwana afanyae mambo haya yote.
18Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu. 19Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi: Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa: 20balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu. 21Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi. 22Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu. 23Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu. 24Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote; 25bassi tumeona vema tukiwa tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paolo, 26watu waliokhatirisha maisha zao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 27Bassi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambieni maneno yayo hayo kwa vinywa vyao. 28Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo illa hayo yaliyo faradhi, 29mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.
30Hatta hao wakiisha kupewa rukhusa wakatelemkia Antiokia; na baada ya kuwakusanya jamii yote wakawapa ule waraka. 31Wakausoma, wakafurahi kwa ajili ya faraja ile. 32Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha. 33Nao wakiisha kukaa huko muda kitambo, wakarukhusiwa na ndugu waende kwa amani kwao waliowatuma. 34Lakini Sila akaona vema kukaa huko. 35Na Paolo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisiia na kulikhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
36Baada ya siku kadha wa kadha Paolo akamwambia Barnaba, Haya! turejee sasa tukawaangalie ndugu katika killa mji tulipolikhubiri neno la Bwana, wa hali gani. 37Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyekwitwa Marko pamoja nao. 38Bali Paolo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfulia, asiende nao kutenda ile kazi. 39Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro. 40Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu. 41Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 15: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.