Matendo 9
9
1LAKINI Saul, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu, 2akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi. 3Hatta alipokuwa akisafiri akawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza nuru kutoka mbinguni. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona wanifukuza? 5Akasema, U nani Bwana? Akasema, Mimi ndimi Yesu unaeniudhi wewe. 6Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda. 7Na watu waliosafiri pamoja nae wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. 8Saul akaondoka katika inchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu: wakamshika mkono wakamleta hatta Dameski. 9Akawa siku tatu haoni, wala hali, wala hanywi.
10Bassi palikuwapo mwanafunzi Dameski, jina lake Anania. Bwana akamwambia katika njozi, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Sawa, ukatafute ndani ya nyumba ya Yuda mtu jina lake Saul, wa Tarso: maana yuko anasali: 12nae amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, akiweka mikono juu yake, apate kuona tena. 13Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia khabari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemi: 14hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. 17Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18Marra yakaanguka machoni pake kama magamba, akapata kuona akasimama, akabatizwa; 19akala chakula, akapata nguvu.
Akawa huko siku kadhawakadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewateka walioliita Jina hili Yerusalemi? Na hapa amekuja kusudi hili, awafunge na kuwapeleka kwa makuhani wakuu? 22Saul akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithubutisha ya kuwa huyu udiye Kristo.
23Hatta siku nyingi zilipopita, Wayahudi wakafanya shauri illi wamwue: 24lakini hila yao ikajulikana na Saul. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua. 25Wanafunzi wakamtwaa usiku wakamshusha ukutani, wakimtelemsha katika kapu.
26Na Saul alipofika Yerusalemi, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. 27Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu. 28Nae akawa pamoja nao katika Yerusalemi akiingia na kutoka. 29Akaneua kwa jina lake Yesu pasipo khofu, akinena na kushindana na Wahelenisti. Nao wakajaribu kumwua. 30Lakini ndugu walipopata khabari wakamchukua hatta Kaisaria wakampeleka Tarso.
31Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
32Hatta Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote akawatelemkia watakatifu waliokaa Ludda. 33Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. 34Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako. 35Marra akaondoka. Na watu wote waliokaa Ludda na Saron wakamwona, wakamgeukia Bwana.
36Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yoppa, jina lake Tabitha, (tafsiri yake ni paa:) mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37Ikawa siku zile akaugua, akafa: hatta walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 38Na kwa kuwa Ludda ulikuwa karibu na Yoppa, nao wamesikia ya kwamha Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi asikawie kuja kwao. 39Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika wakampeleka juu orofani: wajane wote wakasimama karibu nae, wakilia na kuniwonyesha zile kanzu na nguo alizozifanya Paa wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. 41Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi. 42Ikajulikana katika Yoppa, katika mji mzima, watu wengi wakamwamini Bwana. 43Hatta Petro akakaa siku kadha wa kadha huko Yoppa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simon, mtengenezaji wa ngozi.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo 9: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.