Yohana MT. 15
15
1MIMI ndimi niliye mzabibu wa kweli, na Baba yangu ni mkulima. 2Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa. 3Ninyi mmekwisba kuwa safi kwa sababu ya neno nililowaambia. 4Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu. 5Mimi mzabibu; ninyi matawi; akaae ndani yangu, na mimi ndani yake, huyu huzaa Sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno. 6Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea. 7Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa. 8Kwa hiyo atukuzwa Baba yangu, mzae sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9Kama Baba alivyonipenda mimi, nami nimewapenda ninyi; kaeni katika pendo langu. 10Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake. 11Haya nimewaambieni, illi furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 12Amri yangu ndio hii, mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13Hakima aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuweka uzima wake kwa ajili ya rafiki zake. 14Ninyi m rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni. 16Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.
17Haya nawaamuru, mpate kupendana. 18Ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu. 21Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka. 22Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; sasa hawana udhuru kwa dhamhi yao. 23Anichukiae mimi, humchukia na Baba yangu. 24Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. 25Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre. 26Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 15: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.