Yohana MT. 18
18
1ALIPOKWISHA kusema haya, Yesu akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ngʼambu ya kijiti Kedron, palipo bustani; akaingia, yeye na wanafunzi wake. 2Yuda nae, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikwenda huko marra nyingi pamoja na wanafunzi wake. 3Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha. 4Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti. 5Yesu akawaambia, Mimi ndiye. Yuda nae aliyemsaiiti alikuwa akisimama pamoja nao. 6Bassi alipowaambia. Mimi ndiye, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni kwaniba mimi ndiye; bassi mkinitafuta mimi, waacheni hawa waende zao; 9illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao. 10Bassi Simon Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumishi wa kuhani mkuu akamkata sikio lake la kuume. Na yule mtumishi jina lake alikwitwa Malko. 11Bassi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga wako alani mwake. Kikombe alichonipa Baba, nisikinywee? 12Bassi kile kikosi na yule jemadari na wale watumishi wa Wayahudi wakamkamata Yesu, wakanifunga, 13wakamchukua kwa Anna kwanza: maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule. 14Na Kayafa ndiye aliyewapa Wayahudi shauri kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
15Simon Petro akamfuata Yesu, na mwanafunzi mwingine: na yule mwanafunzi alikuwa anajulika na kuhani mkuu: akaingia pamoja na Yesu behewani mwa kuhani mkuu; lakini Petro akasimama nje mlangoni. 16Bassi yule mwanafunzi mwingine aliyejulika na kuhani mkuu akatoka akasema na mwanamke aliye mngoje mlango, akamleta Petro ndani. 17Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi. 18Na wale watumishi na askari walikuwa wamesimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi, wakawa wakikota moto. Petro nae, alikuwa pamoja nao, anakota moto.
19Bassi kuhani mkuu akamwuliza Yesu khabari za wanafunzi wake, na khabari za mafundisho yake. 20Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno. 21Ya nini kumuliza? waulize wale waliosikia, ni nini niliyosema nao: wao wanajua niliyowaambia. 22Aliposema maneno haya, mmoja wa wale watumishi aliyesimama karibu akampiga Yesu koli, akinena, Wamjibu hivi kuhani mkuu? 23Yesu akamjibu, Kama nimesema mabaya, yashuhudie yale mabaya; bali kama nimesema mema, wanipigia nini? 24Bassi Anna akampeleka amefungwa kwa Kayafa kuhani mkuu. 25Na Simon alikuwa akisimama, anakola moto. Bassi wakamwambia, Wewe nawe je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake? Yeye akanena, Sio mimi. 26Mmoja wa wale watumishi wa kuhani mkuu, ni jamaa yule aliyekatwa sikio na Petro, akasema, Mimi sikukuona bustanini pamoja nae? 27Bassi Petro akakana tena, jogoo akawika marra.
28Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka. 29Bassi Pilato akawatokea nje akasema, Mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu? 30Wakajibu, wakamwambia, Kama huyu asingekuwa mtu mwovu, tusingemleta kwako. 31Bassi Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa sharia yenu. Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna rukhusa kuua mtu; 32illi neno lake Yesu litimizwe, alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa.
33Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? 34Yesu akajibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, ama watu wengine walikuambia khabari zangu? 35Pilato akajibu, Je! mimi Myahudi? Taifa lako na makuhani wakuu ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu: watumishi wangu wangalinipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi: lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa. 37Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu. 38Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani?
Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake. 39Lakini kwenu kuna desturi, ya mimi kuwafungulia mtu mmoja wakati wa Pasaka: bassi, wapenda niwafungulie mfalme wa Wayahudi? 40Bassi wakapiga kelele marra ya pili, wote pia, wakinena, Si huyu, bali Barabba. Nae Barabba alikuwa mnyangʼanyi.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 18: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: