Yohana MT. 19
19
1BASSI ndipo Pilato akamtwaa Yesu, akampiga mijeledi. 2Askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi jekundu; wakawa wakimwendea, 3wakisema, Salamu, Mfalme wa Wayahudi! wakimpiga makofi. 4Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake. 5Bassi Yesu akatoka nje, amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi jekundu. Pilato akawaambia, Tazama, Mtu huyu! 6Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake. 7Wayahudi wakamjibu, Sisi tuna sharia, na kwa sharia hiyo amepasiwa kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu. 8Bassi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa; 9akaingia tena Praitorio, akamwamhia Yesu, Umetoka wapi wewe? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10Bassi Pilato akamwambia, Husemi na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukusulibisha na nina mamlaka ya kukufungua? 11Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. 12Tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si mpenda Kaisari; killa ajifanyae kuwa mfalme amfitini Kaisari. 13Bassi Pilato, aliposikia maneno haya, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti, mahali paitwapo Sakafu ya mawe, na kwa Kiebrania Gabbatha. 14Ilikuwa Maandalio ya Pasaka: ilikuwa panapo saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, mfalme wenu! 15Bassi wale wakapiga kelele, Mwondoshe, mwondoshe, msulibishe. Pilato akawaambia, Nimsulibishe mfalme wenu? Makuhani wakuu wakajibu, Hatuna mfalme illa Kaisari. 16Bassi ndipo akamtia mikononi mwao asulibishwe. Bassi wakampokea Yesu: 17akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha; 18wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja nae, huko na huko, na Yesu katikati. 19Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. 20Bassi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali paie aliposulihiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. 21Bassi makuhani wakuu wa Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; hali ya kwamba yule alisema, Mimi mfalme wa Wayahudi. 22Pilato akajihu, Niliyoandika nimeyaandika. 23Bassi askari, walipomsulibisha Yesu, wakatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu mane, kwa killa askari fungu lake; nayo kanzu: na kanzu ile haikushonwa, imefumwa pia tangu juu. 24Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.
25Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. 26Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako. 27Baadae akamwambia mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua kwake. 28Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu. 29Kikawako chombo kimejaa siki; bassi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya husopo, wakampelekea kinywani. 30Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho. 31Bassi Wayahudi, kwa maana ni Maandalio, miili isikae juu va msalaba siku ya sabato (maana siku ya sabato ile ilikuwa siku kuhwa), wakamwomba Pilato, miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. 32Bassi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili aliyesulibiwa pamoja nae. 33Walipomjia Yesu, wakiona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; 34lakini askari mmoja kwa mkuki alimchoma ubavu, ikatoka marra damu na maji. 35Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini. 36Kwa maana haya yalitukia andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena, 37andiko la pili lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. 38Hatta baada ya haya, Yusuf, aliye wa Arimathaya, nae vu mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri (maana aliwaogopa Wayahudi), akamwomba Pilato rukhusa auondoe mwili wake Yesu: Pilato akampa rukhusa. Bassi akaenda akauondoa mwili wake. 39Akaenda Nikodemo nae, yule aliyemwendea usiku hapo kwanza, akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia. 40Bassi wakautwaa mwili wa Yesu, wakaufunga saanda ya bafta, pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. 41Na mahali pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani kaburi jipya, bado hajatiwa mtu aliye yote ndani yake. 42Humo bassi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 19: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: