Yohana MT. 8
8
1lakini Yesu akaenda mlima wa mizeituni. 2Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha. 3Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati, 4wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5Bassi katika torati Musa alituamuru kuwapiga mawe watu kama hao; bassi wewe wasema nini? 6Wakasema neno hili wakimjaribu wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika inchi. 7Nao wakazidi kumhoji, akajiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika inchi. 9Nao, waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianza tangu wazee hatta wa mwisho; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke akisimama katikati. 10Yesu akajiinua asimwone mtu illa yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Hapana aliyekuhukumu? 11Akamwambia, Hapana Bwana. Yesu akamwambia, Nami sikuhukumu. Enenda, wala usitende dhambi tena.
12Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. 13Bassi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia nafsi yako; ushuhuda wako si kweli. 14Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako. 15Ninyi mwahukumu kwa jinsi ya kiwiliwili; mimi simhukumu mtu. 16Na nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli, kwa kuwa mimi si peke yangu bali mimi na Baba aliyenipeleka. 17Na tena katika sharia yenu imeandikwa, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. 18Mimi ndimi ninaejishuhudia nafsi yangu, nae Baba aliyenipeleka ananishuhudia. 19Bassi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mngaliuijua mimi, mngalimjua na Baba yangu.
20Maneno haya aliyasema Yesu akifundisha kakika hekalu, katika chumba cha hazina; wala hapana mtu aliyemkamata, kwa kuwa saa yake ilikuwa haijaja bado.
21Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja. 22Bassi Wayahudi wakanena, Je! atajiua, kwa kuwa anena, Niendako mimi hamwezi kuja? 23Akawaambia, Ninyi wa chini, mimi wa juu; ninyi wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. 24Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. 25Bassi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Neno lilo hilo nisemalo nanyi tangu mwanzo. 26Nina maneno mengi ya kusema na kuhukumu katika khabari zenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu. 27Hawakufahamu ya kuwa awatajia Baba. 28Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo. 29Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo. 30Alipokuwa akisema haya, wengi walimwamini.
31Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli; 32tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru. 33Wakamjihu, Tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wanenaje, Mtawekwa huru? 34Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambieni, Killa atendae dhambi, ni mtumwa wa dhambi. 35Na mtumwa hakai ndani ya nyumba siku zote; mwana hukaa siku zote. 36Bassi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli. 37Najua ya kuwa m mzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu. 38Niliyoyaona kwa Baba yangu udiyo niyanenayo: nanyi vivyo hivyo mliyoyaona kwa baba yenu, ndiyo myatendayo. 39Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ni Ibrahimu. Yesu akawaambia, Kama mugekuwa watoto wa Ibrahimu, mngetenda kazi zake Ibrahimu. 40Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu. 41Wakamwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zina; tuna baba mmoja, yaani Mungu. 42Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma. 43Mbona hamyafahamu maneno yangu haya niyasemayo? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia neno langu. 44Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo. 45Nami, kwa sababu naisema kweli, hamniamini. 46Nani wenu anishuhudiae kuwa nina dhambi? Nikisema kweli, mbona ninyi hamniamini? 47Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu. 48Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo? 49Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu. 50Nami siutafuti ntukufu wangu; yuko atafutae na kuhukumu. 51Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele. 52Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele. 53Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, nae amekufa? Na manabii wamekufa; wajifanya kuwa nani? 54Yesu akajibu, Nikijitukuza nafsi yangu, utukufu wangu si kitu; anitukuzae ni Baba yangu; mmnenae ninyi kuwa ni Mungu wenu. 55Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika. 56Ibrahimu baba yemi alishangilia apate kuiona siku yangu; akaona, akafurahi. 57Bassi Wayahudi wakamwambia. Hujapata bado miaka khamsini, na Ibrahimu umemwona? 58Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo. 59Bassi wakatwaa mawe wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana MT. 8: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.