Luka MT. 17
17
1AKAWAAMBIA wanafunzi wake, Mambo ya kukosesha hayana buddi kutokea, lakini ole wake mtu yule ayaletae! 2Ingemfaa huyu zaidi jiwe la kusagia litiwe shingoni pake akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa hawa wadogo. 3Jihadharini: ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu, msamehe, 4na akikosa marra saba katika siku moja, akakurudia marra saba, akisema, Natubu, msamehe. 5Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu. 6Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini. 7Lakini nani kwenu mwenye mtumishi anaelima, an anaeehunga kondoo? je! amwambia marra atakapoingia, akitoka mashamba, Njoo upesi, keti, ule chakula? 8La! kinyume cha hayo, atamwambia, Pakua chakula, nile; jifunge, unikhudumie hatta nikiisha kula na kunywa; na baada ya haya utakula na kunywa mwenyewe. 9Je! amshukuru yule mtumishi kwa sahahu alifanya alivyoamriwa? Sidhani. 10Kadhalika na ninyi, mkiisha kufanya vyote mlivyoamriwa, semeni, Sisi watumishi wasiofaa; tumetenda yaliyotupasa kutenda. 11Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemi, alikuwa akipita kati ya Samaria na Galilaya. 12Alipokuwa akiingia kijiji kimoja, wakakutana nae watu kumi wenye ukoma, waliosimama mbali; 13nao wakapaaza sauti zao wakisema, Yesu, Bwana, uturehemu. 14Alipowaona, akawaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa katika kwenda kwao wakatakasika. 15Mmoja wao akiona ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; 16akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria. 17Yesu akajiliu, akasema, Si wote kumi waliotakasika? Wale tissa wa wapi? 18Hiawakupatikana waliorudi kumpa Mungu sifa zake, illa mgeni huyu. 19Akamwambia, Simama; enenda zako; imani yako imekuokoa.
20Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu waja lini? akawajibu, akasema, Ufalme wa Mungu hauji kwa kupelelezwa. 21Wala hawatasema, Tazama, huko au huko! maana fahamuni! ufalme wa Mungu umo ndani yenu. 22Akawaambia wanafunzi wake, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku mojawapo ya siku za Mwana wa Adamu wala hamtaiona. 23Na watawaambieni, Tazama huko, au tazama huko! Msiondoke hapo mlipo wala msiwafuate. 24Kwa maana kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hatta upande huu chini ya mbingu, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake. 25Lakini kwanza hana buddi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi biki. 26Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa na katika siku za Mwana wa Adamu. 27Walikuwa wakila, wakinywa, wakioa, wakiozwa, hatta siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, gbarika ikafika, ikawaangamiza wote. 28Vivyo hivyo kama ilivyokuwa siku za Lut: walikuwa wakila, wakinywa, wakimmua, wakiuza, wakipanda, wakijenga; 29hatta siku ile amhayo Lut alitoka Sodom, kukanya moto na kiberiti kutoka mbinguni, vikawaangamiza wote. 30Kadhalika itakuwa katika siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. 31Katika siku ile, aliye juu darini, na vyombo vyake ndani ya nyumba, asishuke illi kuvitwaa: nae aliomo shambani vivyo hivyo asirejee nyuma. 32Mkumbukeni mkewe Lut. 33Mtu ye yote atakaeisalimisha roho yake ataiangamiza, na mtu ye yote atakaeitoa ataihifadhi. 34Nawaambieni, Usiku ule watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa. 35Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja, mmoja atatwaliwa, na mmoja ataachwa. 36Watu wawili watakuwa mashambani; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 37Wakajibu wakamwambia, Wapi, Bwana? Akawaambia, Mzoga uliko ndiko watakakokutana tai.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 17: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: