Luka MT. 18
18
1AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa, 2akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani; hamchi Mungu wala hajali mtu. 3Na katika mji huo palikuwa na mjane aiiyemwendeaendea, akisema, Nipatie haki yangu, ukaniokoe na adui yangu. 4Nae hakukubali muda wa siku kadha wa kadha; khalafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa mimi simchi Mungu wala sijali mtu; 5illakini kwa kuwa mjane huyu ameniudhi, nitampatia haki yake, asije akanidhoofisha kwa kunijia daima. 6Bwana akasema, Sikieni asemavyo yule kadhi asiye haki. 7Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi. 8Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani?
9Yesu akawaambia mfano huu watu waliojidhani nafsi zao kuwa wenye haki, wakiwadharau wengine wote. 10Watu wawili walipanda hekaluni kusali; mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. 11Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru. 12Nafunga marra mbili kwa juma; nalipa zaka za mapato yangu yote. 13Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. 14Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.
15Bassi wakamletea hatta watoto wachanga illi awaguse; lakini wanafunzi wake walipoona wakawakaripia. 16Bali Yesu akawaita waje kwake, akisema, Waacheni watoto waje kwangu, kwa maana watu kama hawo ufalme wa Mungu ni wao. 17Amin, nawaambieni, Yeye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto, hatauingia kamwe.
18Na mtu mkuhwa mmoja akamwuliza, akisema, Mwalimu mwema, nifanyeni nipate kuurithi uzima wa milele? 19Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja ndiye Mungu. 20Wazijua amri, Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudu uwongo, Waheshimu baba yako na mama yako. 21Akasema, Haya yote nimeyashika tangu ujana wangu. 22Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate. 23Lakini aliposikia maneno haya akafanya huzuni nyingi: maana alikuwa mtu tajiri sana.
24Bassi Yesu alipoona ya kuwa amefanya huzuni nyingi, akasema, Kwa shidda gani wenye mali watauingia ufalme wa Mungu. 25Kwa maana ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 26Nao waliposikia, wakasema, Nani, bassi, awezae kuokoka? 27Akasema, Yasiyowezekana kwa wana Adamu, yawezekana kwa Mungu. 28Petro akasema, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. 29Akawaambia, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au wazazi, au ndugu, au mke, au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu, 30illa atapokea zaidi marra nyingi sasa wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
31Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii. 32Kwa maana atatiwa katika mikono ya Mataifa, atafanyiwa dhihaka na kutendwa jeuri, na kutemewa mate; 33na wakiisha kumpiga mijeledi, watamwua; na siku ya tatu atafufuka. 34Nao hawakufahamu haya hatta kidogo, neno hili likawa limefichwa kwao, wala hawakuyajua yaliyonenwa. 35Ikawa alipokaribia Yeriko, pafikuwa na kipofu, amekaa kando ya njia akiomba. 36Aliposikia makutano yanapita, akauliza khabari, Kuna nini? 37Wakamweleza, Yesu wa Nazareti anapita. 38Akapiga kelele, akisema, Yesu, Mwana wa Daud, unirehemu. 39Bassi, waliotangulia wakamkemea, anyamaze; lakini yeye akazidi sana kupiga makelele, Mwana wa Daud, unirehemu. 40Yesu akasimama, akaamuru aletwe kwake; 41na alipomkaribia akamwuliza, Wataka nikufanyie nini? Akasema, Bwami, nipate kuona. 42Yesu akamwambia, Upewe kuona imani yako imekuponya. 43Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 18: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: