Luka MT. 19
19
1AKAINGIA Yeriko akawa akipita katikati yake. 2Na tazama, mtu mmoja, jina lake alikwitwa Zakkayo, mkubwa wa watoza ushuru, nae tajiri: 3akatafuta kumwona Yesu, ni mtu gani, asiweze lakini kwa sababu ya makutano, maana kimo chake alikuwa mfupi. 4Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa sababu alitaka kupita njia ile. 5Na Yesu, alipofika mahali pale, akatazama juu, akamwona, akamwambia, Zakkayo, shuka upesi; maana leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6Akashuka upesi, akamkaribisha kwa furaha. 7Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi. 8Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne. 9Yesu akamwambia, Leo wokofu umefika nyumbani humu, kwa kuwa huyu nae ni mwana wa Ibrahimu. 10Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.
11Nao wakisikia haya akaongeza akawaambia mfano, kwa sababu alikuwa akikaribia Yerusalemi, nao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana marra moja. 12Bassi akasema, Mtu mmoja, mungwana, alisafiri kwenda inchi ya mbali illi kujipatia ufalme na kurejea. 13Akawaita watu kumi katika watumishi wake, akawapa mane za fedha kumi, akawaambia, Fanyeni biashara hatta nitakaporudi. 14Wenyeji wake wakanichukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatutaki mtu huyu atutawale. 15Ikawa aliporejea, baada ya kuupokea ufalme, akatoa amri waitwe wale watumishi aliowapa ile fedha, apate kujua jinsi walivyofanya biashara. 16Wa kwanza akaja akasema, Bwana, mane yako imepata mane kumi. 17Akasema, Vema, mtumishi mwema, kwa sababu umekuwa mwaminifu kwa kitu kilicho kidogo, bassi, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 18Akaja wa pili, akisema, Mane yako, Bwana, imepata mane tano. 19Akamwambia yule nae, Na wewe uwe juu ya miji mitano. 20Akaja mwingine akasema, Bwana, tazama, mane yako hii niliyokuwa nayo, imewekwa akiba katika leso: 21maana nalikuogopa, kwa sababu wewe mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda. 22Akamwambia, Kwa kinywa chako nitakuhukumu, ee mtumishi mwovu wewe. Ulijua ya kuwa mimi mtu mgumu, naondoa nisichoweka, navuna nisichopanda; 23mbona, bassi, hukuweka fedha yangu kwao watoao riba, nami nikija ningaliipata pamoja na faida? 24Akawaambia waliohudhuria, Mnyangʼanyeni mane yake moja mkampe yule mwenye mane kumi. 25(Wakamwambia, Bwana, ana mane kumi). 26Maana nawaambieni, Killa aliye na kitu, atapewa, bali yeye asiye na kitu hatta kile alicho nacho atanyangʼanywa. 27Walakini wale adui zangu wasiotaka niwatawale, waleteni huku mkawachinje mhele zangu.
28Alipokwisha kusema haya, akaendelea mbele, akipanda kwenda Yerusalemi.
29Hatta alipokaribia Bethfage na Bethania karibu ya mlima wa mizeituni, akatuma wawili katika wanafunzi wake, akisema, 30Enendeni zenu hatta kile kijiji kinachowakabili ninyi, na mkiingia ndani, mtaona mwana punda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni. 31Na mtu akiwaambieni, Mbona mnamfungua? semeni hivi, Bwana ana haja nae. 32Bassi, wale waliotumwa wakaenda, wakaona vile vile kama alivyowaambia. 33Na walipokuwa wakimfungua mwana punda, wenyewe wakawauliza, Mnamfunguliani huyu mwana punda? 34Wakasema, Bwana ana haja nae. 35Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya yule mwana punda wakampandisha Yesu. 36Nae alipokuwa akienda, wakatandaza nguo zao njiani. 37Hatta alipokuwa amekwisha kukaribia matelemko va mlima wa mizeituni, kundi lote la wanafunzi wake wakaanza kufurahi na kumhimidi Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona, 38wakinena Amebarikiwa mfalme ajae kwa jina la Bwana, amani mbinguni, na utukufu palipo juu. 39Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wakemee wanafunzi wako. 40Akajibu, akasema, Nawaambieni kwamba, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.
41Nae alipokaribia akauona mji, akaulilia, 42akasema, Laiti ungalijua siku hii yaliyo ya amani! lakini sasa yamefichwa machoni mwenu; 43Kwa maana siku zitakujilia, adui zako watakapokujengea boma; watakuzunguka, watakudhiikisha pande zote; 44watakuangusha chini, na watoto wako ndani yako; wasikuachie jiwe juu ya jiwe; kwa kuwa hukujua majira ya kujiliwa kwako. 45Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wakuzao na wanunuao ndani yake; akiwaambia, 46Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi. 47Akawa akifundisha killa siku hekaluni, makuhani wakuu na waandishi na wakubwa wa watu wakatafuta kumwangamiza, 48nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza.
Iliyochaguliwa sasa
Luka MT. 19: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: