Mattayo MT. 25
25
1NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. 2Watano wao walikuwa wenye busara, ua watauo wapumbavu. 3Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao: 4bali wale wenye busara walitwaa na mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. 5Hatta bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala. 6Hatta usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi anakuja; tokeni kwenda kumlaki. 7Marra wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. 8Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. 9Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakinena, Labuda hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia kwenda kwao wauzao, mkanunue wenyewe. 10Nao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja nae arusini: mlango ukafungwa. 11Khalafu wakaja na wale wanawali wengine, wakinena, Bwana, Bwana, utufungulie. 12Akajibu, akasema, Amin, nawaambieni, siwajui ninyi. 13Bassi kesheni, maana hamwijui siku wala saa ajapo Mwana wa Adamu.
14Maana ni mfano wa mtu atakae kusafiri kwenda inchi ya ugeni, aliwaita watumishi wake, akaweka kwao mali zake. 15Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; killa mtu kwa kadri ya uwezo wake; marra akasafiri. 16Bassi yule aliyepokea talanta tano akashika njia, akafanya kazi nazo, akachuma talanta nyingine tano. 17Vilevile na yule mwenye mbili, yeye nae akachuma nyingine mbili faida.
18Bali yule aliyepokea moja, alikwenda akafukua chini, akaiticha fedha ya bwana wake. 19Baada ya siku nyingi yuaja bwana wa watumishi wale, akafanya hesabu nao. 20Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akinena, Bwana, uliweka kwangu talanta tano: tazama, talanta nyingine tano zaidi nilizopatafaida. 21Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema, na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako. 22Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili: tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. 23Bwana wake akamwambia, Vema, mtumishi mwema na amini: ulikuwa amini kwa machache, nitakuweka juu ya mengi: ingia katika furaha ya bwana wako. 24Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya: 25nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako chini ya inchi: tazama, unayo iliyo yako. 26Bwana wake akajibu, akamwambia, Mtumishi mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27bassi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwao wawekao fedha ya watu; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28Bassi, mnyangʼanyeni talanta yake, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29Kwa maana killa aliye na mali atapewa, na kuongezewa: nae asiye nayo, hatta ile aliyo nayo atanyangʼanywa. 30Na mtumishi yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza ya nje; huko kutakuwa kilio na kusaga meno.
31Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake: 32na mataifa yote watakusanyika mbele yake: nae atawabagua kama vile mchunga abaguavyo kondoo na mbuzi: 33atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu: 35kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37Ndipo wenye haki watakaponijibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38Lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39Lini tulipokuona u mgonjwa, an kifungoni, tukakujia? 40Na mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambieni. Kadiri mlivyomtendea mmojawapo katika hawo ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake: 42kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike: nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44Ndipo hawo pia watajibu, wakinena, Bwana, lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikukhudumu? 45Nae atawajibu, akinena, Amin, nawaambieni, Kadiri msivyomtendea mmojawapo katika hawo walio wadogo, na mimi hamkunitendea. 46Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.
Iliyochaguliwa sasa
Mattayo MT. 25: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.