Mattayo MT. 28:12-15
Mattayo MT. 28:12-15 SWZZB1921
Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi, wakinena, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala. Na jambo hili likisikilikana kwa liwali, tutasema nae, nanyi tutawaondoa shaka. Bassi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno lile likaenea katika Wayahudi hatta leo.