Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko MT. 13

13
1HATTA alipokuwa akitoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, Mwalimu, namna gani ya mawe! namna gani ya majengo! 2Yesu akajibu, akawaambia, Waona majengo haya makuhwa makubwa? Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomelewa.
3Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, kuelekea hekalu, Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea wakamwuliza kwa faragha, Tuambie, haya yatakuwa lini? 4Na nini dalili ya wakati hayo yote yatakapokuwa karibu kutimia?
5Yesu akajibu, akaanza kuwaambia, Jihadharini, mtu asiwadanganye; kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, 6Mimi ndiye: na watadanganya wengi. 7Tena mtakaposikia vita na khabari za vita, msitishwe: maana hayana buddi kutukia, lakini mwisho wenyewe bado. 8Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme utapigana na ufalme: kutakuwa na matetemeko ya inchi mahali mahali; kutakuwa na njaa, na fitina: Hayo ndio mwanzo wa utungu. 9Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao. 10Tena sharti Injili ikhubiriwe kwanza katika mataifa yote. 11Na watakapowachukueni, na kuwateni katika mikono ya watu, msianze kuwaza mtakayosema, wala msishughulike: lakini lo lote mtakalopewa saa ile, lisemeni: kwa maana si ninyi mseniao, hali Roho Mtakatifu. 12Na ndugu atamsaliti ndugu yake illi anawe, na baba mtoto wake, na watoto wataondoka jun ya wazazi wao, na kuwafisha. 13Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kustahimili hatta mwisho, ndiye atakaeokoka. 14Lakini mlionapo chukizo la uharibifu (lile lililoneuwa ua nabii Danieli) likisimama pasipolipasa (asomae na afahamu) ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani; 15nae aliye juu ya dari asishuke nyumbani, wala asiingie kuchukua kitu katika nyumba yake, 16Nae aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake. 17Ole wao wenye mimba, nao wanyonyeshao siku zile! 18Ombeni kukimbilia kwerm kusiwe wakati wa baridi. 19Kwa maana siku zile zitakuwa na shidda jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hatta sasa, wala hazitakuwa kamwe. 20Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile. 21Na wakati huo mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko huko, msisadiki: 22kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule. 23Bali ninyi mwe macho: nimekwisha kuwaonyeni yote mbele.
24Lakini siku hizo baada ya shidda ile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, 25na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. 26Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu. 27Ndipo atakapowatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa inchi hatta upande wa mwisho wa mbingu.
28Kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake liauzapo kuwa laini, na kuchanua majani yake, mwajua ya kuwa karibu wakati wa bari: 29kadhalika na ninyi, myaonapo haya yanatukia, fahamuni ya kuwa ni karibu milangoni. 30Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita kabisa, hatta haya yote yapatapo kuwa. 31Mbingu na inchi zitapita: maneno yangu hayatapita kamwe. 32Lakini khabari ya siku ile na saa ile hakuna aijuae, hatta malaika walio mbinguni, wala Mwana, illa Baba. 33Angalieni, kesheni, ombeni, kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwa. 34Ni kana kwamba mtu mwenye kusafiri, ameacha nyumba yake, amewapa amri watumwa wake, na killa mtu kazi yake, amemwamuru bawabu akeshe. 35Kesheni bassi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au usiku wa manane, au awikapo jogoo, an assubuhi: 36asije akawasili ghafula akawakuta mmelala. 37Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia Wote, Kesheni.

Iliyochaguliwa sasa

Marko MT. 13: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia