Marko MT. 15
15
1MARRA ilipokuwa assubuhi makuhani wakuu wakafanya shauri pamoja na wazee na waandishi na haraza zima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta kwa Pilato. 2Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajihu, akamwambia, wewe unasema. 3Makuhani wakamshitaki mengi. 4Pilato akamwuliza tena akinena, Hujibu neno? Tazama mambo mangapi wanayokushitaki! 5Wala Yesu hakujibu neno tena, hatta Pilato akataajabu. 6Bassi katika siku kuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamtakae. 7Palikuwa na mtu aitwae Barabba, amefungwa pamoja na watu waliofanya fitina na kufanya uuaji katika fitina. 8Makutano wakapaaza sauti zao, wakaanza kuomba vile kama alivvozoea kuwatendea. 9Pilato akawajibu, akisema, Mnataka niwafungulie mfalme wa Wayahudi? 10Kwa maana alifahamu ya kuwa makuhani wakuu wamemtoa kwa husuda. 11Makuhani wakuu wakawataharakisha makutano, illi apende kuwafungulia Barabba. 12Pilato akajibu tena akawaambia, Bassi wataka nimtendeni huyu mnenae kuwa Mfalme wa Wayahudi? 13Wakapiga kelele tena, Msulibishe. 14Pilato akawaambia, Kwani, ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, Msulihishe. 15Pilato akapenda kuwafanyia radhi makutano, akawafungulia Barabba: akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, asulibiwe. 16Askari wakamchukua ndani ya sebule, ndiyo Praitorio, wakakusanya pamoja kikosi kizima. 17Wakamvika vazi jekundu, wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani; 18wakaanza kumsalimu, Salamu Mfalme wa Wayahudi! 19Wakampiga kichwa kwa unyasi, wakamtemea mate, wakapiga magoti, wakamsujudu. 20Hatta wakiisha kumdhihaki, wakamvua lile vazi jekundu, wakamvika nguo zake mwenyewe; wakamchukua nje wamsulibishe. 21Wakamtumikisha mtu aliyekuwa akipita, Simon Mkurene, akitoka mashamba, baba wa Iskander na Rufo, auchukue msalaba wake. 22Wakamleta mahali palipokwitwa Golgotha, tafsiri yake, mahali pa kichwa. 23Wakampa mvinyo iliyotiwa manemane anywe, nae hakupokea. 24Wakamsulibi, wakagawanya nguo zake wakizipigia kura killa mtu atwae nini. 25Ikawa saa tatu wakamsulibi. 26Anwani ya mshitaka wake iliandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDU. 27Na pamoja nae walisulibi wanyangʼanyi wawili, mmoja mkono wake wa kuume na mmoja mkono wake wa kushoto. 28Bassi andiko likatimizwa linenalo, Alihesabiwa pamoja na maasi. 29Nao waliopita wakamtukana, wakitikisatikisa vichwa vyao, wakisema, Ah! wewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, 30jiponye nafsi yako, shuka msalabani. 31Kadhalika na makuhani wakuu wakamdhihaki wao kwa wao, pamoja na waandishi, wakisema, Aliwaponya wengine; hawezi kujiponya nafsi yake. 32Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu, 33Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza juu ya inchi yote, hatta saa tissa. 34Na saa tissa Yesu akapiga kelele kwa sauti kuu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? tafsiri yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
35Na baadhi yao waliohudhuria, wakisikia, wakasema, Anamwita Eliya. 36Mtu akapiga mbio, akajaza sifongo siki, akaitia jim ya unyasi, akamnywesha, akisema, Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumshusha. 37Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38Pazia la patakatifu likapasuka vipande viwili toka juu hatta chini. 39Bassi yule akida, aliyesimama akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa, Mwana wa Mungu.
40Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; katika hawa alikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama wa Yakobo mdogo na wa Yose, na Salome: 41hawa ndio waliomfuata alipokuwa Galilaya, na kumkhudumia; na wengine wengi waliopanda pamoja nae hatta Yerusalemi.
42Hatta ikiisba kuwa jioni, kwa sababu ni Maandalio, ndiyo siku iliyo kabla ya sabato, 43akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu. 44Pilato akastaajabu, kwa sababu amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo. 45Hatta alipokwisha kupata hakika, akamtunukia Yusuf maiti. 46Akanunua saanda, akamshusha, akamfungia ile saanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani: akafingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi. 47Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yose wakapatazama alipowekwa.
Iliyochaguliwa sasa
Marko MT. 15: SWZZB1921
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.

: