Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko MT. 16

16
1HATTA sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu wa Yakobo na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. 2Hatta assubuhi mapema, siku ya kwanza ya sabato, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza; 3wakasemezana wao kwa wao, Nani atakaetufingirishia lile jiwe kutoka mlangoni mwa kaburi? 4Hatta walipotazama, wakaona ya kuwa lile jiwe limekwisha kufingirishwa; nalo lilikuwa kubwa nmo.
5Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu. 6Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka. 7Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya: huko mtamwona, kama alivyowaambia. 8Wakatoka humo, wakakimbia kutoka kaburini: kwa maana waliingia tetemeko na ushangao: wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.
9Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba. 10Huyu akashika njia akawapa khabari wale waliokuwa pamoja nae tangu zamani, wangali wakiomboleza na kulia. 11Na hawa waliposikia kama yu hayi akaonwa nae, hawakusadiki. 12Baada ya haya akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. 13Na hawa wakaenda zao wakawapa khabari wale wengine: wala hawakuwasadiki hawa.
14Baadae akaonekana na wale edashara walipokuwa wakila, akawalaumu kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki waliomwona alipofufuka. 15Akawaambia, Enendem nlimwenguni mwote, mkaikhubiri injili kwa killa kiumbe. 16Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; Kwa jina langu watafukuza pepo; watasema kwa ndimi mpya; 18watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. 19Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20Nao wakatoka, wakakhubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithubutishia neno kwa ishara zilizofuatana nalo. Amin.

Iliyochaguliwa sasa

Marko MT. 16: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia