2 Mose 10:21-23
2 Mose 10:21-23 SRB37
Bwana akamwambia Mose: Uinue mkono wako na kuuelekeza mbinguni, katika nchi ya Misri kuwe giza jeusi sana la kupapaswa. Mose alipouinua mkono wake na kuuelekeza mbinguni, kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri siku tatu. Mtu hakuweza kumwona mwenziwe, wala mtu hakuondoka siku tatu mahali, alipokuwa. Lakini kwao wana wa Israeli kulikuwa na mwanga po pote, walipokaa.