Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mose 10

10
Pigo la nne: Nzige.
1Bwana akamwambia Mose: Nenda kwake Farao! Kwani mimi nimeushupaza moyo wake nayo mioyo ya watumishi wake, nipate kuvitoa hivi vielekezo vyangu katikati yao, 2kusudi wewe uyasimulie masikioni mwa mwanao namo mwa mjukuuu wako, niliyoyafanya huku Misri, navyo vilekezo vyangu, nilivyoviweka kwao, mpate kujua, ya kuwa mimi ni Bwana.#2 Mose 6:2-7. 3Mose na Haroni walipofika kwake Farao wakamwambia: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Waebureo: Mpaka lini utakataa kujinyenyekeza usoni pangu? Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!#2 Mose 5:3. 4Kwani utakapokataa kuwapa ruhusa kwenda zao walio ukoo wangu, utaniona, nikileta nzige kesho katika mipaka yako. 5Nao wataifunika nchi hapo juu, watu wasiweze kuona mchanga, nao watayala masazo yenu yote yaliyosazwa kwa kuiponea mvua ya mawe, nayo miti yenu yote iliyochipuka tena wataila mashambani. 6Watajaa namo nyumbani mwako namo manyumbani mwa watumishi wako, namo manyumbani mwa Wamisri wote; ajabu kama hilo hawakuliona baba zako, wala baba za baba zako tangu hapo, walipoanza kuwapo katika nchi hii hata siku hii ya leo. Kisha akageuka, akatoka kwake Farao.
7Ndipo, watumishi wake Farao walipomwambia: Mpaka lini mtu huyu atatunasa? Watu hawa wape ruhusa kwenda zao, wamtumikie Bwana Mungu wao! Hujatambua bado, ya kuwa Misri imekwisha kuangamia? 8Kwa hiyo Mose na Haroni wakarudishwa kwake Farao, naye akawaambia: Nendeni kumtumikia Bwana Mungu wenu! Lakini watakaokwenda ni nani na nani? 9Mose akajibu: Tunakwenda vijana wetu na wazee wetu, wana wetu wa kiume na wa kike, nao mbuzi na kondoo wetu na ng'ombe wetu tutakwenda nao, kwani tuna sikukuu ya Bwana.#2 Mose 5:1. 10Lakini akawaambia: Ehe! Bwana na awe nanyi vivyo hivyo, kama nitakavyowapa ruhusa kwenda zenu pamoja na watoto wenu! Yatazameni mabaya, mliyo nayo, myafuate! 11Hivyo sivyo! Ila nendeni ninyi waume kumtumikia Bwana! Kwani hii ndiyo, mnayoitaka. Kisha wakawafukuza, watoke usoni pake Farao.
12Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Uinue mkono wako juu ya nchi ya Misri, nzige waje! Nao na waiingie nchi ya Misri, wale majani yote ya nchi hii nayo yote pia, mvua ya mawe iliyoyasaza.#2 Mose 9:32. 13Mose alipoiinua fimbo yake juu ya nchi ya Misri, Bwana akaleta upepo toka maawioni kwa jua, nao ukavuma katika nchi hiyo mchana kutwa na usiku kucha; kulipokucha, huo upepo wa maawioni kwa jua ulikuwa umewaleta nzige. 14Nao hawa nzige wakaiingia nchi yote ya Misri, wakatua po pote katika mipaka ya Misri, nao walikuwa wakali sana wa kula; nzige kama hao walikuwa hawajatokea siku zilizopita, wala hawatatokea siku zijazo. 15Wakaifunikiza nchi yote pia hapo juu, hata nchi ikapata giza; wakayala majani yote ya nchi nayo matunda yote ya miti, mvua ya mawe iliyoyasaza, hakukusalia jani moja tu penye miti wala penye vijiti vya mashambani katika nchi yote ya Misri. 16Ndipo, Farao alipomwita kwa upesi Mose na Haroni, akawaambia: Nimemkosea Bwana Mungu wenu, hata ninyi.#2 Mose 9:27. 17Sasa uniondolee nayo mara hii kosa langu, mniombee kwa Bwana Mungu wenu, aniondolee kifo hiki tu!#2 Mose 8:12; 1 Sam. 12:19. 18Alipotoka kwake Farao, akamwomba Bwana.#4 Mose 11:2. 19Ndipo, Bwana alipoleta upepo mwingine toka baharini wenye nguvu sana, ukawainua wale nzige, ukawapeleka na kuwatosa katika Bahari Nyekundu, asisalie nzige hata mmoja katika mipaka yote ya Misri. 20Kisha Bwana akaushupaza moyo wa Farao, asiwape wana wa Isiraeli ruhusa kwenda zao.#2 Mose 4:21.
21Bwana akamwambia Mose: Uinue mkono wako na kuuelekeza mbinguni, katika nchi ya Misri kuwe giza jeusi sana la kupapaswa. 22Mose alipouinua mkono wake na kuuelekeza mbinguni, kukawa na giza nene katika nchi yote ya Misri siku tatu. 23Mtu hakuweza kumwona mwenziwe, wala mtu hakuondoka siku tatu mahali, alipokuwa. Lakini kwao wana wa Israeli kulikuwa na mwanga po pote, walipokaa. 24Ndipo, Farao alipomwita Mose, akamwambia: Nendeni kumtumikia Bwana! Mbuzi na kondoo na ng'ombe tu waachwe huku, lakini wana wenu na waende nayi!#2 Mose 10:10. 25Mose akamwambia: Sharti wewe mwenyewe utupe mikononi mwetu ng'ombe za tambiko za kuchinja nazo za kuteketeza nzima, tupate za kumtolea Bwana Mungu wetu. 26Kwa hiyo, nayo makundi yetu sharti yaende nasi, lisisalie hata kwato moja. Kwani humo ndimo, tutakamochukua za kumtambikia Bwana Mungu wetu; kwani sisi hatujui, jinzi tutakavyomtumikia Bwana, mpaka tufike huko. 27Lakini Bwana akaushupaza moyo wa Farao, akatae kuwapa ruhusa kwenda zao.#2 Mose 4:21. 28Kwa hiyo Farao akamwambia: Ondoka kwangu! Jiangalie, usitokee tena kuuona uso wangu! Kwani siku, utakapouona uso wangu, utakufa. 29Mose akajibu: Na viwe hivyo, ulivyosema, nisiuone tena uso wako mara nyingine.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mose 10: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia