2 Mose 11
11
Mungu anawaagiza Waisiraeli, wajiweke tayari kutoka Misri.
1Bwana akamwambia Mose: Liko pigo moja bado, nitakalompatia Farao nao Wamisri, baadaye atawapa ninyi ruhusa kutoka huku; naye hapo, atakapowapa ruhusa kwenda zenu na mali zenu zote, atawakimbiza ninyi kabisa kuondoka huku. 2Kwa hiyo sema masikioni mwa watu hawa, waombe vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu kila mtu kwa mwenziwe, hata kila mwanamke kwa mwenziwe.#2 Mose 3:21-22. 3Bwana atawapatia hawa watu upendeleo machoni pao Wamisri, maana huyo Mose alikuwa mkubwa sana katika nchi ya Misri machoni pao watumishi wa Farao napo machoni pa watu.
Mose analifumbua pigo la kumi litakalokuwa.
4Mose akasema: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana: Usiku wa manane nitatokea katikati ya nchi ya Misri; 5ndipo, kila mwana wa kwanza atakapokufa katika nchi ya Misri, kuanzia mwana wa kwanza wa Farao anayekaa katika kiti chake cha kifalme, kuishia mwana wa kwanza wa kijakazi anayekaa penye mawe ya kusagia, hata kila mwana wa kwanza wa nyama wa kufuga.#2 Mose 4:23. 6Ndipo, maombolezo yatakapokuwa makuu katika nchi yote ya Misri yasiyokuwa bado siku zilizopita, wala hayatakuwa kama hayo siku zijazo. 7Lakini kwa wana wote wa Isiraeli mbwa tu hatakemea wala mtu wala nyama, kusudi mpate kujua, ya kuwa Bwana huwapambanua Wamisri na Waisiraeli.#2 Mose 9:4,26. 8Ndipo, hawa watumishi wako wote watakapotelemka, waje kwangu na kuniangukia kwamba: Toka wewe na hawa watu wote wanaozifuata nyayo zako! Ndipo, nitakapotoka. Kisha Mose akatoka kwake Farao kwa kuwa na ukali uliowaka moto.
9Kisha Bwana akamwambia Mose: Farao hatawasikia ninyi, kusudi vifanyike vioja vyangu vingi katika nchi ya Misri. 10Nao Mose na Haroni walipovifanya hivyo mbele ya Farao, Bwana akaushupaza moyo wa Farao, asiwape wana wa Isiraeli ruhusa kutoka katika nchi yake.#2 Mose 4:21.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 11: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.