ndipo, kila mwana wa kwanza atakapokufa katika nchi ya Misri, kuanzia mwana wa kwanza wa Farao anayekaa katika kiti chake cha kifalme, kuishia mwana wa kwanza wa kijakazi anayekaa penye mawe ya kusagia, hata kila mwana wa kwanza wa nyama wa kufuga. Ndipo, maombolezo yatakapokuwa makuu katika nchi yote ya Misri yasiyokuwa bado siku zilizopita, wala hayatakuwa kama hayo siku zijazo.