Nami nitapita usiku uleule katika nchi yote ya Misri, nimpige kila mwana wa kwanza katika nchi ya Misri aliye wa wwatu pamoja nao walio wa nyama wa kufuga, nayo miungu yote ya Misri nitaihukumu mimi Bwana. Nazo zile damu penye nyumba mlimo zitakuwa kielekezo chenu: nitakapoziona nitapita kwenu, lisiwapate ninyi lile pigo la mwangamizaji, nitakapoipiga nchi ya Misri.