Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mose 13

13
Wazaliwa wa kwanza ni wake Bwana.
1Bwana akamwambia Mose kwamba: 2Kila mtoto mume atakayezaliwa wa kwanza na mama yake ye yote, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga kwao wana wa Isiraeli, sharti amtoe kuwa wangu mimi. Kwani ni wangu kweli.#4 Mose 8:17-18; 18:15; Luk. 2:23.
Agizo la kula mikate isiyochachwa.
3Mose akawaambia hao watu: Ikumbukeni siku hii ya leo kuwa ndiyo, mliyotoka huko Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa! Kwani Bwana amewatoa huko kwa mkono wenye uwezo, siku hiyo kisiliwe cho chote chenye chachu. 4Siku hii ndiyo, mliyotoka nayo katika mwezi wa Abibu.#2 Mose 12:2. 5Napo hapo, Bwana atakapokupeleka katika nchi yao Wakanaani na Wahiti na Waamori na Wahiwi na Wayebusi, aliyowaapia baba zako kukupa wewe, katika ile nchi ichuruzikayo maziwa na asali, huko shari uuangalie utumishi huu, uutumikie katika mwezi huu!#1 Mose 17:8. 6Siku saba ule mikate isiyochachwa, nayo siku ya saba iwe ya sikukuu yenyewe!#2 Mose 12:15-16. 7Mikate isiyochachwa iliwe siku saba, isionekane kwako wala mikate iliyochachwa wala chachu yo yote katika mipaka yako!#1 Kor. 5:8. 8Nao wanao na uwaeleze siku hiyo kwamba: Ni kwa kuwa Bwana alitufanyia haya na haya, tulipotoka kule Misri. 9Nayo sharti yawe kwako kielekezo mkononi pako na ukumbusho katikati ya macho yako, Maonyo ya Bwana yapate kuwa kinywani mwako, kwani Bwana amekutoa huko Misri kwa mkono wenye uwezo.#5 Mose 6:8; 11:18. 10Nayo maongozi haya sharti uyaangalie, uyafuate, siku zao zitakapotimia mwaka kwa mwaka!
Agizo la kumtolea Bwana wana wa kwanza.
11Hapo Bwana atakapokuingiza katika nchi ya Kanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, akakupa, iwe yako, 12ndipo umtolee Bwana kila atakayezaliwa wa kwanza na mama yake naye kila mwana wa nyama wa kufuga atakayekuwa wa kwanza, utakayempata, wao wa kiume watakuwa wake Bwana. 13Kila mwana wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo; usipomkomboa mvunje shingo! Naye kila mwana wa kwanza wa mtu kwao wanao utamkomboa. 14Tena kama mwanao atakuuliza kesho kwamba: Haya maana yake nini? utamwambia: Bwana alitutoa kwa mkono wenye uwezo kule Misri nyumbani, tulimokuwa watumwa.#2 Mose 12:26. 15Farao alipojishupaza, asitupe ruhusa kwenda zetu, Bwana aliwaua wana wote wa kwanza katika nchi ya Misri, wao waliokuwa wana wa kwanza wa watu nao waliokuwa wana wa kwanza wa nyama wa kufuga; kwa hiyo ninamtolea Bwana wana wao wote wanaozaliwa wa kwanza wa mama zao walio wa kiume, nao wana wa kwanza wa wanangu ninawakomboa.#2 Mose 12:29. 16Haya na yawe kielekezo mkononi pako, yafungwe napo pajini pako katikati ya macho yako! Kwani Bwana alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
Kutoka Misri kunaendelea.
17Farao alipokwisha kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, Mungu hakuwashikisha njia ya kupita katika nchi ya wafilisti iliyokuwa fupi, kwani Mungu alisema: Labda watu hawa watageuza miyo kwa kuona vita, warudi Misri. 18Kwa hiyo Mungu akawazungusha hao watu na kuwashikisha njia ya nyikani kwenye Bahari Nyekundu. Nao wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri walikuwa wenye mata. 19Mose akaichukua nayo mifupa ya Yosefu kwenda nayo, kwani yeye aliwaapisha wana wa Isiraeli kwamba: Hapo, Mungu atakapowakagua ninyi, sharti mwichukue mifupa yangu, mwitoe huku kwenda nayo.#1 Mose 50:25; Yos. 24:32.
20Walipoondoka Sukoti wakapiga makambi Etamu kwenye mpaka wa hiyo nyika. 21Naye Bwana akawaongoza akiwatangulia mchana kwa wingu jeusi lililokuwa kama nguzo, awaongoze njia, tena usiku kwa moto uliokuwa kama nguzo, uwamulikie, wapate kwenda mchana na usiku.#2 Mose 40:34; 4 Mose 9:15-23; 1 Kor. 10:1. 22Ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana mbele yao hao watu, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku mbele yao.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mose 13: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia