2 Mose 14
14
Waisiraeli wanamaliza kutoka Misri.
1Bwana akasema na Mose kwamba: 2Waambie wana wa Isiraeli, warudi, wapige makambi ya kuelekea Pi-Hahiroti katikati ya Migidoli na baharini; hapo panapoelekea Baali-Sefoni ndipo, mpige makambi karibu ya baharini. 3Ndipo, Farao atakapowawazia wana wa Isiraeli kwamba: Wao wamekwisha kutatanishwa katika nchi hiyo, nayo nyika imewafungia njia, wasitoke. 4Nami nitaushupaza moyo wa Farao, ajihimize kuwafuata, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana. Basi, wakafanya hivyo.#2 Mose 4:21; 9:16; Ez. 28:22.
Farao anawafuata Waisirali.
5Mfalme wa Misri alipopashwa habari, ya kama wale watu wamekimbia, ndipo, moyo wake Farao, nayo mioyo ya watumishi wake ilipogeuka kuwataka tena wale watu, wakasema: Hapo tumefanya nini, tukiwapa Waisiraeli ruhusa kwenda zao na kuziacha kazi za kututumikia sisi? 6Kisha akalitengeneza gari lake, akawachukua nao watu wake kwenda naye, 7tena akachukua magari ya vita 600 yaliyochaguliwa na magari yote yaliyopatikana huko Misri, nao wakuu, aliowatia katika kila gari lake. 8Maana Bwana alikuwa ameushupaza moyo wake Farao, mfalme wa Misri, ajihimize kuwafuata wana wa Isiraeli, ijapo Waisiraeli walitoka kwa nguvu za mkono ulioko juu.#2 Mose 13:9. 9Wamisri wakawafuata na kupiga mbio, farasi na magari yote ya Farao na wapanda farasi wake na vikosi vyake, wakawafikia kwenye bahari, walikopiga makambi, huko Pi-Hahiroti kuelekea Baali-Sefoni.
10Farao alipofika karibu, wana wa Isiraeli wakayainua macho yao, wakawaona Wamisri, walivyofuata nyuma; ndipo, waliposhikwa na woga kabisa, wakampigia Bwana makelele wao wana wa Isiraeli. 11Naye Mose wakamwambia: Kumbe kule Misri hakuna makaburi, ukituchukua, tujifie huku nyikani? Ni kwa sababu gani ukitufanyizia haya kwa kututoa Misri? 12Neno hili silo, tulilokuambia huko Misri kwamba: Tuache, tuwatumikie Wamisri? Kwani inatufalia zaidi kuwatumikia Wamisri kuliko kujifia nyikani. 13Lakini Mose akawaambia hao watu: Msiogope! Jipeni mioyo! Ndipo, mtakapouona wokovu wa Bwana, atakaowapatia leo; kwani hawa Wamisri, mnaowaona leo, hamtawaona tena kale na kale. 14Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza tu.#5 Mose 1:30; 2 Mambo 20:15; Yes. 30:15.
Waisiraeli wanapita baharini.
15Bwana akamwambia Mose: Unanipigiaje makelele? Waambie wana wa Isiraeli, waondoke! 16Wewe nawe iinue fimbo yako na kuikunjulia bahari mkono wako, uitenge! Ndivyo, wana wa Isiraeli watakavyopita pakavu katikati ya bahari. 17Nami utaniona, nikiishupaza mioyo ya Wamisri, waingie nao na kuwafuata ninyi, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, kwa magari yake na kwao wapanda farasi wake.#2 Mose 14:4. 18Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana, nikijipatia utukufu kwake Farao na kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake. 19Kisha malaika wa Mungu aliyekuwa akiwatangulia vikosi vya Waisiraeli akaondoka kwenda nyuma yao, nalo wingu lililokuwa kama nguzo likaondoka mbele yao, likaenda kusimamama nyuma yao,#2 Mose 13:21. 20likatua hapo katikati ya makambi ya Wamisri na makambi ya Waisiraeli; huko likawa wingu lenye giza, lakini huku likauangaza usiku; kwa hiyo hawakuweza kukaribiana wale na hao usiku kucha. 21Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, Bwana akaiendesha bahari kwa nguvu ya upepo uliotoka upande wa maawioni kwa jua na kuvuma kabisa usiku wote, akaipwelesha bahari kuwa pakavu, maji yakigawanyika. 22Ndipo, wana wa Isiraeli walipopaingia pale pakavu katikati ya bahari, maji ya bahari yakawa kama ukuta kuumeni na kushotoni kwao.#Yos. 4:23; Yes. 11:15-16; 1 Kor. 10:1; Ebr. 11:29.
Wamisri wanaangamia baharini.
23Wamisri wakawafuata mbiombio, farasi wa Farao na magari yake nao walioyapanda, wote pia wakaingia nyuma yao humo katikati ya bahari.#2 Mose 15:19. 24Asubuhi kulipopambazuka, Bwana akavichungulia vikosi vya Wamisri toka lile wingu lenye moto na giza, akavistusha vikosi vya Wamisri#Sh. 34:17; 104:32. 25akaiondoa magurudumu ya magari yao na kuyarusha kwa nguvu. Ndipo, Wamisri walipoambiana: Na tuwakimbie Waisiraeli! Kwani Bwana anawapigania, sisi Wamisri tushindwe.#2 Mose 14:14; Sh. 64:10. 26Lakini Bwana akamwambia Mose: Ikunjulie bahari mkono wako, maji yarudiane na kuwatosa Wamisri na magari yao pamoja nao walioyapanda! 27Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, ndipo, maji ya bahari yalipourudia mwendo wake wa siku zote, nayo yalifanyika, kulipopambazuka. Nao Wamisri walipokimbia wakapatwa nayo; ndivyo, Bwana alivyowakumba Wamisri kuingia katikati ya bahari. 28Maji yakarudiana na kuyafunikiza magari pamoja nao waliopanda farasi, ndio vikosi vyote vya Farao walioingia baharini na kuwafuata Waisiraeli, hakusalia kwao hata mmoja. 29Lakini wana wa Isiraeli walipita pakavu katikati ya bahari, maji yakiwasimamia kama ukuta kuumeni na kushotoni kwao.#2 Mose 14:22. 30Ndivyo, Bwana alivyowaokoa siku ile mikononi mwao Wamisri, kisha Waisiraeli wakaiona mizoga ya Wamisri ufukoni kwenye bahari. 31Waisiraeli walipoliona tendo hili kubwa, mkono wa Bwana ulilowafanyizia Wamisri, ndipo, watu hao walipomwogopa Bwana, wakamtegemea Bwana naye mtumishi wake Mose.#2 Mose 19:9; 2 Mambo 20:20.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 14: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: