2 Mose 15
15
Shangilio la Mose la kumshukuru Mungu.
1Hapo ndipo, Mose na wana wana Isiraeli walipomwimbia Bwana wimbo huu, wakasema kwamba:
Na nimwimbie Bwana! Kwani ni mtukufu mno,
Farasi pamoja nao waliowapanda amewatosa baharini.#Ufu. 15:3.
2Bwana ni uwezo wangu na wimbo wangu, hunipatia wokovu.
Yeye ni Mungu wangu, kwa hiyo na nimsifu,
ni Mungu wa baba yangu, kwa hiyo na nimtukuze!#Sh. 118:14; Yes. 12:2.
3Bwana ni mpiga vita, Bwana ni Jina lake.#2 Mose 14:14; 3:15; Sh. 46:10.
4Magari ya Farao na vikosi vyake amewabwaga baharini,
wateule wake wakuu wametoswa katika Bahari Nyekundu;
5vilindi vikawafunika, wakazama chini kama mawe.
6Mkono wako wa kuume, Bwana, hutukuka
kwa nguvu, unazozifanya,
mkono wako wa kuume, Bwana, huwaponda adui.
7Kwa wingi wa ukuu wako unawaangamiza wao wakuinukiao;
ukiyafungua makali yako; huwateketeza kama majani makavu.#Yes. 47:14.
8Kwa kufoka kwa pua yako maji yakakwezwa juu,
mawimbi yakasimama, kama yamo chunguni.
vilindi vikaganda moyoni mwa bahari.
9Adui aliposema: Nijihimize kufuata! Nitafika,
roho yangu itapata kushiba, nikigawanya nyara;
nitauchomoa upanga wangu, mkono wangu uwaangamize:
10ndipo, ulipouvumisha upepo wako,
nayo bahari ikawafunikiza,
wakazama kama risasi katika maji makuu.
11Miongoni mwa miungu yuko nani
anayefanana na wewe, Bwana?
Yuko nani anayefanana na wewe
kwa utukufu na kwa utakatifu?
Anayetisha kwa matendo yanayoshangiliwa,
naye akifanya vioja?#2 Mose 18:11; Sh. 72:18-19.
12Ulipoukunjua mkono wako wa kuume, nchi ikawameza.
13Umewaongoza kwa huruma yako hao watu, uliowakomboa,
ukawafikisha kwa nguvu zako huko, utukufu wako unakokaa.
14Makabila ya watu walipovisikia wakatetemeka;
uchungu ukawapata wenyeji wa Ufilisti.#Yos. 2:9,11.
15Ndipo, wakuu wa Edomu walipostuka nao,
nao madume wa Moabu wakapigwa bumbuazi,
nao wenyeji wa Kanaani wakayeyuka wote.
Mastuko na maogofyo yakawaangukia,
16wakanyamaza kimya kama mawe kwa ukuu wa mkono wako,
mpaka wapite wao walio ukoo wako, Bwana,
mpaka wapite wao wa ukoo huo, uliowakomboa.
17Waingize na kuwapanda kwenye milima iliyo fungu lako,
ulikotengeneza Kao la kukalia wewe Bwana,
ililolisimika mikono yako, Bwana, kuwa Patakatifu.
18Bwana atakuwa mfalme kale na kale.#Sh. 93:1. 19Kwani farasi wa Farao na magari yake pamoja nao walioyapanda walipoingia baharini, Bwana akayarudisha maji ya bahari juu yao, wana wa Isiraeli walipokwisha kupita pakavu katikati ya bahari.#2 Mose 14:22-29. 20Ndipo, mfumbuaji wa kike Miriamu, umbu lake Haroni, alipochukua patu mkononi mwake, nao wanawake wote wakatoka, wamfuate na kupiga patu na kucheza ngoma.#Sh. 68:26.
21Naye Miriamu akawaitikia kwamba:
Mwimbieni Bwana! Kwani ni mtukufu mno,
Farasi pamoja nao waliowapanda amewatosa baharini!#2 Mose 15:1.
Safari ya Waisiraeli: Maji machungu yanageuzwa kuwa matamu.
22Kisha Mose akawasafirisha Waisiraeli na kuwaondoa kwenye Bahari Nyekundu, wakatoka hapo, wakaingia katika nyika ya Suri, wakaenda siku tatu pasipo kuona maji. 23Kisha wakafika Mara, lakini hawakuweza kuyanywa yale maji ya Mara, kwani yalikuwa machungu; kwa hiyo wakapaita mahali pale Mara (Uchungu). 24Ndipo, watu walipomnung'unikia Mose kwamba: Tunywe nini? 25Naye alipomlilia Bwana, Bwana akamwonyesha mti; alipoutupa mti huo majini, maji yakawa matamu. Hapo Bwana akawatolea maongozi yapasayo, akawajaribu hapo 26akiwaambia: Kama utaisikia sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yanyokayo machoni pake na kuyategea maagizo yake masiko yako na kuyaangalia maongozi yake yote, ndipo, utakapoona, ya kuwa sikutii yale magonjwa yote, niliyowatia Wamisri, kwani mimi Bwana ni mponya wako.#5 Mose 7:15; 32:39; Mat. 9:12.
27Kisha wakafika Elimu palipokuwa visima vya maji 12 na mitende 70, wakapiga makambi hapo penye maji.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 15: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: