2 Mose 20
20
Maagizo matakatifu kumi.
1Mungu akayasema maneno haya yote kwamba:#5 Mose 5:6-22; Mat. 5:17-48. 2Mimi ndimi Bwana Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa. 3usiwe na miungu mingine ila mimi!#5 Mose 6:4-5; 1 Kor. 8:6. 4Usijifanyie kinyago wala mfano wo wote wa vitu vilivyoko mbinguni juu, wala vilivyoko nchini chini, wala vilivyomo majini chini ya nchi!#3 Mose 26:1; 5 Mose 27:15; Sh. 97:7; Yes. 40:18-26; Rom. 1:23. 5Usivitambikie, wala usivitumikie! Kwani mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu; manza za baba nitazipatilizia wana, nikifikishe kizazi cha tatu na cha nne, kwao wanichukiao.#2 Mose 34:7; Yer. 31:29-30; Ez. 18:2-3,20. 6Lakini nitawafanyizia mema, nikifikishe hata kizazi cha maelfu, kwao wanipendao na kuyashika maagizo yangu.
7Usilitaje Jina la Bwana Mungu wako bure! Kwani Bwana hatamwachilia alitajaye Jina lake bure.#3 Mose 24:16; 2 Mose 16:25; Ez. 20:12.
8Ikumbuke siku ya mapumziko kuitakasa! 9Siku sita sharti ufanye kazi, uyamalize mambo yako yote!#Mar. 2:27-28; Kol. 2:16-17. 10Lakini siku ya saba ndiyo ya kumpumzikia Bwana Mungu wako. Hapo usifanye kazi yo yote, wala wewe, wala mwanao wa kiume, wala wa kike, wala mtumishi wako wa kiume, wala wa kike, wala nyama wako wa kufuga, wala mgeni wako aliomo malangoni mwako. 11Kwani siku sita Bwana alizifanya mbingu na nchi na bahari navyo vyote vilivyomo, akapumzika siku ya saba; kwa hiyo Bwana aliibariki siku ya saba, akaitakasa.#1 Mose 2:2-3.
12Mheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi, akupayo Bwana Mungu wako!#Mat. 15:4; Ef. 6:2-3. 13Usiue!#2 Mose 21:12; 1 Mose 9:5-6; Yak. 2:11. 14Usizini!#3 Mose 20:10. 15Usiibe!#Ef. 5:3-5. 16Usimshuhudie mwenzio uwongo!#3 Mose 19:11; Ef. 4:28. 17Usiitamani nyumba ya mwenzio!
Usimtamani mke wa mwenzio, wala mtumishi wake wa kiume
wala wa kike, wala ng'ombe wake, wala punda wake,
wala cho chote, mwenzio alicho nacho!#2 Mose 23:1; Ef. 4:25; Rom. 7:7; 13:9.
18Nao watu wote walipoziona zile ngurumo na umeme na mlio wa baragumu nao mlima uliotoka moshi, walipoviona hivi vyote wakakimbia, wakasimama mbali, 19wakamwambia Mose: Sema wewe na sisi, nasi tutasikia! Lakini Mungu asiseme nasi, tusife. 20Naye Mose akawaambia: Msiogope! Kwani Mungu amekuja kuwajaribu ninyi, kusudi mwone na macho yenu, anavyoogopesha, mwache kumkosea. 21Kwa hiyo watu wakasimama mbali, lakini Mose akalikaribia lile wingu jeusi, Mungu alimokuwa.
Mungu anaagiza, jinsi watakavyomtambikia.
22Bwana akamwambia Mose: Hivi ndivyo, uwaambie wana wa Isiraeli: Ninyi mmeona, ya kuwa nimesema nanyi toka mbinguni.#Ebr. 12:18. 23Kwa hiyo msifanye vyo vyote kuwa Mungu kama mimi, msijifanyizie miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu! 24Unijengee kwa udongo pa kunitambikia, upate pa kunitolea ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukruni za kondoo wako na za ng'ombe wako! Napo po pote, nitakapokukumbusha Jina langu, nitakuja kwako, nikubariki.#2 Mose 27:1-8; 29:42-43; 5 Mose 12:5. 25Nawe utakaponijengea kwa mawe pa kunitambikia, usitumie mawe ya kuchonga. Kwani ukiyapiga tu kwa chuma chako cho chote umekwisha kuyatia uchafu.#5 Mose 27:5; Yos. 8:31. 26Tena usitumie ngazi ya kupapandia hapo pa kunitambikia, ni kwamba vyako vyenye soni visifunuliwe hapo pake.
Iliyochaguliwa sasa
2 Mose 20: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: