Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mose 21

21
Mambo ya watumwa.
1Haya ndiyo maamuzi, utakayoyaweka mbele yao:#3 Mose 25:39-40. 2Ukinunua mtumwa wa Kiebureo, sharti atumike miaka sita, lakini katika mwaka wa saba atatoka utumwani pasipo kukombolewa.#5 Mose 15:12-17; Yer. 34:14. 3Kama aliingia kwako peke yake tu, na atoke hivyo peke yake tu; kama aliingia mwenye mkewe, mkewe na atoke utumwani pamoja naye. 4Kama bwana wake alimpa mwanamke, naye akazaa wana wa kiume na wa kike, yule mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wao, naye mume atatoka utumwani peke yake. 5Lakini mtumwa atakaposema: Nampenda bwana wangu na mke wangu na watoto wangu, sitaki kutoka utumwani, 6bwana wake na amtokeze kwa Mungu na kumfikisha penye mlango au penye mwimo, kisha bwana wake na alitoboe hapo sikio lake kwa shazia; ndipo, atakapokuwa mtumwa wake kale na kale.#2 Mose 22:8-9,28; 5 Mose 15:17; Sh. 82.
7Mtu akimwuza mwanawe wa kike kuwa kijakazi, hatatoka utumwani, kama waume wanavyotoka.#2 Mose 21:2. 8Akiwa mbaya machoni pa bwana wake aliyemtaka wa kulala naye, na amtoe, akombolewe; lakini hana ruhusa ya kumwuza kwa watu wa kabila geni, kwani ni yeye aliyemdanganya. 9Lakini akimpa mwanawe wa kiume kuwa wa kulala naye, sharti amfanyizie zile haki zipasazo mwanawe wa kike. 10Akijichukulia mwingine, yule asimkatie wala kitoweo chake wala nguo zake wala ngono zake. 11Asipompatia hayo mambo matatu, atatoka utumwani bure tu pasipo kulipa fedha.
Maagizo yapasayo wauaji
12Mtu akimpiga mwenzake, hata afe, hana budi kuuawa kabisa.#1 Mose 9:6; 2 Mose 20:13; Mat. 5:21-22. 13Lakini kama hakumvizia, ikiwa Mungu amemtia mkononi mwake, nitakuonyesha mahali, atakapopakimbilia.#4 Mose 35:6-29; 5 Mose 19:4-13; 1 Fal. 2:29,31. 14Lakini mtu akimnyatia mwenzake, kusudi apate kumwua kwa kumdanganyadanganya, huyo sharti umtoe hata mezani pangu pa kutambikia, auawe. 15Atakayempiga baba yake au mama yake sharti auawe kabisa. 16Naye atakayemwiba mwenziwe, kama amekwisha kumwuza, au kama anaonekana angalimo mikononi mwake, sharti auawe kabisa.#5 Mose 24:7; 1 Tim. 1:10. 17Naye atakayemwapiza bba yake na mama yake sharti afe kwa kuuawa.#5 Mose 27:17; Fano. 20:20; Mat. 15:4.
Maagizo yapasayo wenye kuwaumiza wenzao.
18Watu wakigombana, mmoja akimpiga mwenzake jiwe au konde, asife, ila augue tu na kulala kitandani, 19naye akipata kuinuka tena na kujiendea nje kwa kujiegemeza na mkongojo, basi, yule aliyempiga asipatwe na jambo lo lote, atamlipa tu siku za kukaa bure pasipo kufanya kazi, nayo mauguzi hana budi kuyalipa.
20Mtu akimpiga fimbo mtumwa wake au kijakazi wake, naye akifa papo hapo, anapomshika kwa mkono wake, sharti alipizwe. 21Lakini akiwapo baadaye siku moja au mbili, hatalipizwa, kwani ni mali yake yeye.
22Watu wakigombana, tena hapo wakipiga mwanamke mwenye mimba, nayo mimba yake ikiharibika pasipo kumtia ugonjwa, sharti atozwe fedha, kama mumewe yule mwanamke atakavyomtakia; hana budi kuzitoa zizo hizo, waamuzi watakazomwagiza. 23Lakini akipata kuumizwa zaidi, sharti umtoze roho kwa roho, 24jicho ka jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,#3 Mose 24:19-20; 5 Mose 19:21; Mat. 5:38. 25kuugua kwa kuugua, kidonda kwa kidonda, vilio kwa vilio.
26Mtu akimpiga mtumwa au kijakazi wake jicho na kuliharibu, sharti ampe ruhusa ya kutoka utumwani kwa kumlipa hilo jicho. 27Hata akimvunja mtumwa au kijakazi wake jino, sharti ampe ruhusa kutoka utumwani kwa kumlipa jino.
28Ng'ombe akimkumba mwanamume au mwanamke kwa pembe zake, akifa, sharti huyo ng'ombe auawe kwa kupigwa mawe, nyama zake zisiliwe, lakini mwenye ng'ombe hana neno. 29Lakini kama huyo ng'ombe alikuwa akikumba watu tangu siku nyingi, naye bwana wake alikuwa ameonywa, lakini hakumwangalia huyo ng'ombe, naye akiua mwanamume au mwanamke, basi, huyo ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe, naye bwana wake hana budi kuuawa.#1 Mose 9:5. 30Lakini akitozwa fedha tu za kujikomboa, sharti azitoe zote, anazotakiwa, ziwe makombozi ya roho yake. 31Ng'ombe akikumba mtoto wa kiume au mtoto wa kike kwa pembe zake, sharti ahukumiwe vivyo hivyo. 32Lakini ng'ombe akikumba mtumwa au kijakazi kwa pembe zake, mwenye ng'ombe sharti amlipe bwana wao fedha 30, naye ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe.
Maagizo ya kuangalia nyama wa kufuga wa wengine.
33Mtu akiacha shimo wazi au akichimba shimo pasipo kulifunikiza, kisha ng'ombe au punda akitumbukia humo, 34mwenye shimo sharti alipe fedha za kumrudishia yule bwana mali zake, kisha nyama aliyekufa atakuwa wake.
35Ng'ombe wa mtu akimkumba ng'ombe wa mwenzake kwa pembe zake, akafa, basi, watamwuza yule ng'ombe aliye mzima, lakini fedha, watakazozipata, sharti wazigawanye, naye ng'ombe aliyekufa sharti wamgawanye. 36Lakini kama ilikuwa imejulikana, ya kuwa huyo ng'ombe hukumba kwa pembe zake tangu siku nyingi, naye bwana wake hakumwangalia, sharti alipe ng'ombe aliye mzima mahali pake al iyekufa, kisha huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa wake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mose 21: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia