2 Mose 8:18-19
2 Mose 8:18-19 SRB37
Waganga nao walipofanya hivyo, watokeze mbu kwa uganga wao, hawakuweza; nao wale mbu wakawauma watu na nyama. Ndipo, walipomwambia Farao: Hiki ndicho kidole chake Mungu! Lakini moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.