Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mose 8

8
Pigo la pili: Vyura wengi.
1Kisha Bwana akamwambia Mose: Nenda kwa Farao, umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!#2 Mose 5:1. 2Lakini wewe utakapokataa kuwapa ruhusa kwenda zao, utaniona mimi, nikiipiga mipaka yako yote na kuleta vyura, 3huo mto ufurikiwe na vyura, nao watapanda, waingie nyumbani mwako namo chumbani mwako mwa kulalia, hata kitandani pako, namo nyumbani mwao watumishi wako, namo vijumbani mwao watu wako, namo majikoni mwako, namo mabakulini mwa kutengenezea mikate. 4Kisha watapanda hao vyura namo mwilini mwako, namo miiilini mwa watu wako wote, namo miilini mwa watumishi wako wote.
5Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Ukunjue mkono wako wenye fimbo yako na kuuelekezea vijito na mito na maziwa, upandishe vyura, waijie nchi ya Misri. 6Haroni alipoukunjua mkono wake na kuuelekezea maji ya Misri, ndipo, vyura walipopanda, wakaifunika nchi ya Misri. 7Waganga nao wakavifanya kwa uganga wao, wakapandisha vyura, waijue nchi ya Misri.#2 Mose 7:11.
8Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Niombeeni kwa Bwana, awaondoe hawa vyura kwangu na kwa watu wangu! Ndipo, nitakapowapa ruhusa watu wa ukoo huu kwenda zao, wamtambikie Bwana.#2 Mose 8:32; 9:28; 10:17. 9Mose akamwambia Farao: Kwa utukufu wako niambie sawasawa, kama ni lini, unapotaka, niwaombee ninyi, wewe na watumishi wako na watu wako, hawa vyura waondolewe kabisa kwako namo manyumbani mwako, wasalie mtoni tu. 10Akasema: Kesho. Akajibu: Itakuwa, kama ulivyosema, upate kujua, ya kuwa hakuna anayefanana na Bwana Mungu wetu.#2 Mose 9:14; 15:11. 11Hawa vyura wataondoka kwako na manyumbani mwako, namo mwao watumishi wako, namo mwao watu wako, wasalie mtoni tu. 12Kisha Mose na Haroni wakatoka kwake Farao, naye Mose akamlilia Bwana kwa ajili ya hao vyura, aliompatia Farao. 13Bwana akafanya, kama Mose alivyosema: vyura wakafa manyumbani na nyuani na mashambani, 14wakawakusanya machungu machungu, nchi ikanuka vibaya. 15Lakini Farao alipoona, ya kuwa jambo limetulia, akaushupaza moyo wake, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.#2 Mose 4:21.
Pigo la tatu: Mbu wengi.
16Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Inyanyue fimbo yako, uyapige mavumbi ya chini, yageuke kuwa mbu katika nchi yote ya Misri! 17Wakafanya hivyo; Haroni alipoukunjua mkono wake wenye fimbo yake na kuyapiga mavumbi ya chini, yakageuka kuwa mbu, wakawauma watu na nyama; mavumbi yote ya nchi yakageuka kuwa mbu katika nchi yote ya Misri. 18Waganga nao walipofanya hivyo, watokeze mbu kwa uganga wao, hawakuweza; nao wale mbu wakawauma watu na nyama.#2 Mose 9:11. 19Ndipo, walipomwambia Farao: Hiki ndicho kidole chake Mungu! Lakini moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.#2 Mose 14:25; 4:21.
Pigo la nne: Mainzi wabaya.
20Bwana akamwambia Mose: Kesho asubuhi na mapema ujidamke, upate kumtokea Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Ndipo umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!#2 Mose 5:1. 21Hawa watu walio ukoo wangu usipowapa ruhusa kwenda zao, utaniona, nikituma kwenu, wewe na watumishi wako na watu wako, namo manyumbani mwako mainzi wabaya, nyumba za Misri nazo nchi, wanazozikaa, zijae hao mainzi wabaya. 22Lakini nchi ya Goseni, wao walio ukoo wangu wanayoikaa, nitaitenga siku hiyo, hao mainzi wabaya wasiweko huko, kusudi upate kujua, ya kuwa mimi Bwana niko katikati ya nchi hiyo.#2 Mose 7:5. 23Hivyo nitawatenga wao walio ukoo wangu nao walio wako; hiki kielekezo kitafanyika kesho. 24Bwana akavifanya hivyo: mainzi wabaya na wakubwa wakaingia nyumbani mwa Farao namo manyumbani mwa watumishi wake na katika nchi yote ya Misri, nayo nchi ikaharibika kwa ajili ya hao mainzi wabaya. 25Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Nendeni kumtambikia Mungu wenu katika nchi hii! 26Lakini Mose akamwambia: Haiwezekani kuvifanya hivyo; kwani tukimtambikia Bwana Mungu wetu, ingewachukiza Wamisri; nao watakapotuona, tukichinja machoni pao ng'ombe za tambiko zinazowachukiza, hawatatupiga mawe?#1 Mose 43:32. 27Sharti twende nyikani safari ya siku tatu, tupate kumtambikia Bwana Mungu wetu, kama alivyotuambia.#2 Mose 3:18. 28Ndipo, Farao aliposema: Basi, mimi nitawapa ninyi ruhusa kwenda kumtambikia Bwana Mungu wenu nyikani. Ninataka hili tu: msiende mbali zaidi, tena: mniombee.#2 Mose 8:12. 29Naye Mose akasema: Tazama! Nikitoka kwako nitamwomba Bwana, hawa mainzi wabaya waondoke kesho kwake Farao nako kwao watumishi wake na watu wake, lakini Farao asiendelee kutudanganya, akikataa tena kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, wapate kumtambikia Bwana! 30Mose alipotoka kwake Farao, akamwomba Bwana.#2 Mose 8:16. 31Naye Bwana akafanya, kama Mose alivyosema: Wale mainzi wabaya wakaondoka kwake Farao nako kwao watumishi wake na watu wake, hakusalia hata mmoja. 32Lakini Farao akaushupaza moyo wake nayo mara hii, hakuwapa hao watu ruhusa kwenda zao.#2 Mose 4:21.

Iliyochaguliwa sasa

2 Mose 8: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia