1
2 Mose 8:18-19
Swahili Roehl Bible 1937
Waganga nao walipofanya hivyo, watokeze mbu kwa uganga wao, hawakuweza; nao wale mbu wakawauma watu na nyama. Ndipo, walipomwambia Farao: Hiki ndicho kidole chake Mungu! Lakini moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
Linganisha
Chunguza 2 Mose 8:18-19
2
2 Mose 8:1
Kisha Bwana akamwambia Mose: Nenda kwa Farao, umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!
Chunguza 2 Mose 8:1
3
2 Mose 8:15
Lakini Farao alipoona, ya kuwa jambo limetulia, akaushupaza moyo wake, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
Chunguza 2 Mose 8:15
4
2 Mose 8:2
Lakini wewe utakapokataa kuwapa ruhusa kwenda zao, utaniona mimi, nikiipiga mipaka yako yote na kuleta vyura
Chunguza 2 Mose 8:2
5
2 Mose 8:16
Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Inyanyue fimbo yako, uyapige mavumbi ya chini, yageuke kuwa mbu katika nchi yote ya Misri!
Chunguza 2 Mose 8:16
6
2 Mose 8:24
Bwana akavifanya hivyo: mainzi wabaya na wakubwa wakaingia nyumbani mwa Farao namo manyumbani mwa watumishi wake na katika nchi yote ya Misri, nayo nchi ikaharibika kwa ajili ya hao mainzi wabaya.
Chunguza 2 Mose 8:24
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video