1 Mose 22
22
Aburahamu anamtoa Isaka kuwa ng'ombe ya tambiko.
1Ikawa, mambo hayo yalipomalizika, Mungu akamjaribu Aburahamu, akamwambia: Aburahamu! naye akajibu: Mimi hapa!#Ebr. 11:17; Yak. 1:12. 2Akamwambia: Mchukue mwana wako wa pekee, umpendaye, huyo Isaka, uende naye katika nchi ya Moria, umtoe huko kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima juu ya mlima mmoja, nitakaokuonyesha!#2 Mambo 3:1. 3Basi, kesho yake Aburahamu akaamka na mapema, akamtandika punda wake, akachukua na vijana wawili kwenda naye, tena mwanawe Isaka; alipokwisha kuchanja nazo kuni za kuchomea ng'ombe ya tambiko, akaondoka kwenda mahali pale, Mungu alipomwambia. 4Aburahamu alipoyainua macho yake siku ya tatu akapaona mahali pale, pangaliko mbali. 5Ndipo, Aburahamu alipowaambia wale vijana wake: Kaeni hapa pamoja na punda! Mimi na huyu kijana tutakwenda huko kutambika, kisha tutarudi kwenu. 6Aburahamu akazichukua zile kuni za kuchomea ng'ombe ya tambiko, akamtwika mwanawe Isaka, naye mwenyewe akashika moto na kisu mkononi mwake, wakaenda hivyo wao wawili pamoja. 7Isaka akamwmbia baba yake Aburahamu: Baba! Akajibu: Mimi hapa, mwanangu! Akasema: Tazama! Moto na kuni tunazo, lakini mwana kondoo wa kuwa ng'ombe ya tambiko yuko wapi? 8Aburahamu akasema: Mwanangu, Mungu atajipatia mwana kondoo wa kuwa ng'ombe ya tambiko. Kisha wakaenda hivyo wao wawili pamoja. 9Walipofika mahali pale, Mungu alipomwambia, Aburahamu akajenga hapo pa kutambikia, akazitandika kuni juu yake; kisha akamfunga mwanawe Isaka, akamweka hapo pa kutambikia juu ya hizo kuni; 10kisha Aburahamu akaukunjua mkono wake, akakishika kisu cha kumchinjia mwanawe.#Yak. 2:21. 11Ndipo, malaika wa Bwana alipomwita toka mbinguni kwamba: Aburahamu! Aburahamu! Akaitikia: Mimi hapa! 12Akamwambia: Usimkunjulie mtoto mkono wako! Usimfanyizie cho chote! Kwani sasa nimejua, ya kuwa unamwogopa Mungu, maana hukumnyima hata mwanao wa pekee.#Yer. 7:31; Rom. 8:32. 13Aburahamu alipoyainua macho yake akaona kulungu nyuma yake aliyekamatwa pembe zake na kichaka; huyo kulungu akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko mahali pake mwanawe. 14Aburahamu akapaita mahali hapo: Bwana aona; kwa hiyo watu husema hata leo: Mlimani, Bwana anakoonwa.
Aburahamu anabarikiwa.
15Malaika wa Bwana akamwita Aburahamu toka mbinguni mara ya pili, 16akasema: Ndivyo, asemavyo Bwana: Nimejiapia kwamba: Kwa kuwa umelifanya jambo hili, usininyime mwanao wa pekee,#Ebr. 6:13. 17nitakubariki kweli, nikupe, uzao wako uwe watu wengi sana kama nyota za mbinguni au kama mchanga ulioko ufukoni kwenye bahari, hao wa uzao wako wayatwae malango ya adui zao kuwa yao.#1 Mose 13:16; 15:5; Ebr. 11:12; 1 Mose 24:60. 18Katika uzao wako ndimo, mataifa yote ya nchini yatakamobarikiwa, kwa kuwa umeisikia sauti yangu.#1 Mose 12:3; 26:4; Gal. 3:16. 19Kisha Aburahamu akarudi kwa wale vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja kwenda Beri-Seba; kule Beri-Seba ndiko, Aburahamu alikokaa.
Vizazi vya Nahori.
20Mambo hayo yalipomalizika, Aburahamu akapashwa habari kwamba: Tazama, naye Milka amemzalia ndugu yako Nahori wana.#1 Mose 11:29. 21Mwanawe wa kwanza ni Usi, ndugu yake ni Buzi, tena Kemueli, baba yao Washami, 22na Kesedi na Hazo na Pildasi na Idilafu na Betueli. 23Naye Betueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia ndugu yake Aburahamu hao wanane,#1 Mose 24:15. 24naye suria yake aliyeitwa Ruma akamzaa Teba, tena Gahamu na Tahasi na Maka.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 22: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.