1 Mose 35
35
Yakobo anakwenda Beteli.
1Mungu akamwambia Yakobo: Inuka, upande kwenda Beteli kukaa huko! Tena jenga huko pa kumtambikia Mungu aliyekutokea huko, ulipomkimbia kaka yako Esau!#1 Mose 28:12-19; 31:13. 2Ndipo, Yakobo alipowaambia wao wa mlango wake nao wote, aliokuwa nao: Iondoeni miungu migeni iliyo kwenu bado! Kisha jieueni na kuvaa nazo nguo nyingine!#1 Mose 31:19; Yos. 24:23; 1 Sam. 7:3. 3Kisha na tuondoke, tupande kwenda Beteli, nijenge huko pa kumtambikia Mungu aliyeniitikia siku ile, nilipokuwa nimesongeka, akawa pamoja na mimi katika safari hiyo, niliyokwenda.#1 Mose 28:15,20-22. 4Ndipo, walipompa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, nayo mapete ya masikioni mwao, naye Yakobo akayafukia chini ya mkwaju uliokuwa karibu ya Sikemu.#Yos. 24:26; Amu. 9:6. 5Walipoondoka, kitisho cha Mungu kikaiguia ile miji yote iliyowazunguka, wasiwakimbize wana wa Yakobo na kuwafuata. 6Ndivyo, yakobo alivyofika Luzi katika nchi ya Kanaani, ndio Beteli, yeye pamoja na watu wote, aliokuwa nao. 7Akajenga huko pa kutambikia, akapaita mahali pale Mungu wa Beteli, kwani ndiko, Mungu alikomtokea, alipomkimbia kaka yake.#1 Mose 12:8. 8Siku zile akafa Debora aliyekuwa yaya wake Rebeka, akazikwa upande wa chini hapo Beteli chini ya mvule, nao ukaitwa Mvule wa Maombolezo.#1 Mose 24:59.
Yakobo anaitwa Isiraeli, kisha anabarikiwa.
9Mungu akamtokea Yakobo tena, aalipokwisha kurudi Mesopotamia, akambariki. 10Hapo Mungu akamwambia: Jina lako ni Yakobo, lakini usiitwe tena jina lako Yakobo, ila jina lako liwe Isiraeli! Kwa hiyo wakamwita Isiraeli.#1 Mose 32:28. 11Kisha Mungu akamwambia: Mimi ni Mungu Mwenyezi; na uzae wana, upate kuwa wengi, taifa na kundi zima la mataifa litatoka kwako, nao wafalme watatoka kiunoni mwako.#1 Mose 17:1; 28:3-4; 17:6. 12Nayo nchi hii, niliyompa Aburahamu na Isaka, nakupa wewe nawe, nao wa uzao wako wajao nyuma yako nitawapa nchi hii. 13Kisha Mungu akapaa juu na kutoka kwake mahali hapo, aliposema naye.#1 Mose 17:22. 14Mahali hapo, aliposema naye, Yakobo akapasimamisha nguzo, nayo nguzo hiyo ilikuwa ya mawe, akaimwagia kinywaji cha tambiko, kisha akaipaka mafuta juu yake.#1 Mose 28:18-19. 15Yakobo akapaita jina lake mahali hapo, Mungu aliposema naye, Beteli.
Kufa kwake Raheli.
16Kisha wakaondoka Beteli. Ikawa, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, Raheli akazaa, nako huko kuzaa kwake kukawa kugumu. 17Hapo, machungu yake ya kuzaa yalipozidi, mzalishaji akamwambia: Usiogope! Kwani nayo mara hii utazaa mtoto mume. 18Ikawa roho yake ilipomtoka kwa kupatwa na kufa, akamwita jina lake Benoni (Azimalizaye nguvu zangu), lakini baba yake akamwita Benyamini (Mbahati). 19Ndivyo, Raheli alivyokufa, akazikwa hapohapo penye njia ya kwenda Efurata, ndio Beti-Lehemu.#Mika 5:1. 20Yakobo akasimamaisha juu ya kaburi lake nguzo ya mawe, nayo nguzo hiyo iko juu ya kaburi la Raheli hata siku ya leo.
21Kisha Isiraeli akaondoka, akalipiga hema lake ng'ambo ya huko ya mnara wa Ederi.#Mika 4:8. 22Ikawa, Israeli alipokaa katika nchi ile, Rubeni akaenda, akalala na Biliha, suria ya baba yake; naye Isiraeli akavisikia.#1 Mose 49:4.
Wana wa Yakobo.
23Wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili. Wana wa Lea ni wanawe wa kwanza wa Yakobo: Rubeni, tena Simeoni na Lawi na Yuda na Isakari na Zebuluni. 24Wana wa Raheli ni Yosefu na Benyamini. 25Nao wana wa Biliha, kijakazi wake Raheli, ni Dani na Nafutali. 26Nao wana wa Zilpa, kijakazi wake Lea, ni Gadi na Aseri. Hawa ndio wana wa Yakobo, aliozaliwa huko Mesopotamia.
Kufa kwake Isaka.
27Kisha Yakobo akafika kwa baba yake Isaka kule Mamure karibu ya Kiriati-Arba, ndio Heburoni, aburahamu na Isaka walikokaa ugenini. 28Nazo siku zake Isaka zilikuwa miaka 180. 29Ndipo, Isaka alipozimia, akafa, akachukuliwa kwenda kwao walio wa ukoo wake; naye alikuwa mkongwe mwenye siku za kushiba siku za kuwapo. Kisha wanawe Esau na Yakobo wakamzika.#1 Mose 25:8.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 35: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: