1 Mose 36
36
Vizazi vya Esau.
(Taz. 1 Mambo 1:35-54.)
1Hivi ndivyo vizazi vyake Esau aliyeitwa Edomu:#1 Mose 25:30. 2Esau akachukua wakeze kwao wanawake wa Kanaani: Ada, binti Mhiti Eloni, na Oholibama, binti Ana, binti Mhiwi Siboni,#1 Mose 26:34. 3na Basimati, binti Isimaeli, umbu lake Nebayoti.#1 Mose 28:9. 4Ada akamzalia Esau Elifazi, naye Basimati akamzaa Reueli. 5Naye Oholibama akamzaa Yeusi na Yalamu na Kora.
6Kisha Esau akawachukua wakeze na wanawe wa kiume na wa kike nao wote waliokuwa nyumbani mwake na mbuzi na kondoo wake na nyama wengine wote, aliowafuga, na mapato yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani, akaondoka kwa ndugu yake Yakobo, akaenda katika nchi nyingine. 7Kwani mapato yao yalikuwa mengi, wasiweze kukaa pamoja; nayo nchi hiyo, waliyoikaa ugeni, haikuweza kuwaeneza kwa ajili ya makundi yao.#1 Mose 13:6. 8Kwa hiyo Esau akaenda kukaa vilimani kwa Seiri, naye Esau ndiye Edomu.
9Navyo hivi ndivyo vizazi vyake Esau, baba yao Waedomu, milimani kwa Seiri. 10Haya ndiyo majina yao wanawe Esau: Elifazi, mwana wa Ada, mkewe Esau, tena Reueli, mwana wa Basimati, mkewe Esau. 11Nao wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo na Gatamu na Kenazi. 12Naye Timuna alikuwa suria yake Elifazi, mwana wa Esau; akamzalia Elifazi Amaleki. Hawa ndio wana wa Ada, mkewe Esau. 13Nao hawa ndio wana wa Reueli: Nahati na Zera, Sama na Miza; hawa ndio wana wa Basimati, mkewe Esau. 14Nao hawa ndio wana wa Oholibama, binti Ana, binti Siboni, mkewe Esau, aliomzalia Esau: Yeusi na Yalamu na Kora.
15Hawa ndio majumbe wao wana wa Esau: Wana wa Elifazi, mwanawe wa kwanza wa Esau, walikua: Jumbe Temani, jumbe Omari, jumbe Sefo, jumbe Kenazi, 16jumbe Kora, jumbe Gatamu, jumbe Amaleki. Hawa ndio majumbe wa Elifazi katika nchi ya Edomu, nao ndio wana wa Ada. 17Nao hawa ndio wana wa Reueli, mwana wa Esau: Jumbe Nahati, Jumbe Zera, Jumbe Sama, jumbe Miza. Hawa ndio majumbe wa Reueli katika nchi ya Edomu, nao ndio wana wa Basimati, mkewe Esau. 18Nao hawa ndio wana wa Oholibama, mkewe Esau: Jumbe Yeusi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hawa ndio majumbe wa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau. 19Hawa ndio wanawe Esau, nao ndio majumbe wao. Hawa ndio Waedomu.
20Hawa ndio wana wa Mhori Seiri waliokuwa katika hiyo nchi: Lotani na Sobali na Siboni na Ana,#1 Mose 14:6; 5 Mose 2:12. 21na Disoni na Eseri na Disani; hawa ndio majumbe wa Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu. 22Nao wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemamu, naye umbu lake Lotani ni timuna. 23Nao hawa ndio wana wa Sobali: Alwani na Manahati na Ebali, Sefo na Onamu. 24Nao hawa ndio wana wa Siboni: Aya na Ana; huyu Ana ndiye aliyeziona chemchemi za maji ya moto nyikani alipowachunga punda wa baba yake Siboni. 25Nao hawa ndio wana wa Ana: Disoni na Oholibama, binti Ana. 26Nao hawa ndio wana wa Disoni: Hemudani na Esibani na Itirani na Kerani. 27Hawa ndio wana wa Eseri: Bilihani na Zawani na Akani. 28Hawa ndio wana wa Disani: Usi na Arani. 29Hawa ndio majumbe wa Wahori: Jumbe Lotani, jumbe Sobali, jumbe Siboni, jumbe Ana, 30jumbe Disoni, jumbe Eseri, jumbe Disani; hawa ndio majumbe wa Wahori walioushika ujumbe wao katika nchi ya Seiri.
31Nao hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, wana wa Isiraeli walipokuwa hawajapata bado mfalme. 32Bela, mwana wa Beori, alikuwa mfalme huko Edomu, nalo jina la mji wake ni Dinihaba. 33Bela alipokufa, Yobabu, mwana wa Zera aliyetoka Bosira, akawa mfalme mahali pake. 34Yobabu alipokufa, Husamu wa nchi ya Watemani akawa mfalme mahali pake. 35Husamu alipokufa, Hadadi, mwana wa Bedadi aliyewapiga Wamidiani katika mbuga za Wamoabu, akawa mfalme mahali pake; nalo jina la mji wake ni Awiti. 36Hadadi alipkufa, Samula aliyetoka Masireka akawa mfalme mahali pake. 37Samula alipokufa, Sauli aliyetoka Rehoboti wa Mtoni akawa mfalme mahali pake. 38Sauli alipokufa, Baali-Hanani, mwana wa Akibori, akawa mfalme mahali pake. 39Baali-Hanani, mwana wa Akibori, alipokufa, Hadari akawa mfalme mahali pake, nalo jina la mji ni Pau, nalo jina la mkewwe ni Mehetabeli, binti Matiredi, binti Mezahabu.
40Haya ndiyo majina ya majumbe wa Esau, tena ndivyo, walivyoitwa majina yao kwa ndugu zao napo mahali pao, walipokaa: Jumbe Timuna, jumbe Alwa, jumbe Yeteti, 41jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni, 42jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibusari, 43jumbe Magidieli, jumbe Iramu. Hawa ndio majumbe wa Waedomu, jinsi walivyoitwa kwa koo zao katika hizo nchi, walizozichukua kuwa zao. Huyu ndiye Esau, baba yao Waedomu.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 36: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: