1 Mose 43
43
Safari ya pili ya kaka zake Yosefu kwenda Misri pamoja na Benyamini.
1Njaa ikawa nzito katika nchi. 2Walipokwisha kuzila hizo ngano, walizozileta toka Misri, baba yao akawaambia: Rudini huko kutununulia vilaji vichache! 3Ndipo, Yuda alipomwambia kwamba: Yule mtu alitushuhudia kwa ukali kwamba: Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi. 4Ukitaka kumtuma huyu ndugu yetu kwenda pamoja na sisi, tutatelemka kukununulia vilaji; 5lakini usipotaka kumtuma, hatuwezi kutelemka, kwani yule mtu alituambia: Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi. 6Ndipo, Isiraeli aliposema: Kwa nini mmenifanyizia haya mabaya ya kumpasha yule mtu habari, ya kuwa yuko ndugu yenu mwingine? 7Wakajibu: Yule mtu alituuliza mara kwa mara habari za kwetu na za udugu wetu kwamba: Baba yenu yuko mzima bado? Mna ndugu mwingine? Nasi hatukuwa na budi kumjibu hayo maulizo yake; tungalijuaje, ya kuwa anataka kutuambia: Sharti mmtelemshe ndugu yenu?#1 Mose 42:7-13. 8Naye Yuda akamwambia baba yake Isiraeli: Mtume huyu kijana kwenda na mimi, tupate kuondoka kwenda huko, tupone, tusife sisi na wewe na watoto wetu. 9Mimi na niwe mdhamini wake, na umtafute mkononi mwangu! Nisipomrudisha na kumsimamisha mbele yako nitakuwa nimekukosea siku zote. 10Kama hatungalikawilia, tungalikuwa tumekwisha kurudi hata mara mbili. 11Basi, baba yao Isiraeli akawaitikia kwamba: Kama hayana budi kuwa hivyo, haya! Yafanyizeni! Chukueni vyomboni mwenu mazao ya nchi hii yanayosifiwa, tena mpelekeeni yule mtu kuwa matunzo yake: mafuta ya mkwaju machache na asali kidogo na manukato na uvumba na kungu na lozi!#Fano. 18:16. 12Tena chukueni mikononi mwenu fedha za mara mbili, nazo fedha zile zilizorudishwa katika magunia yenu sharti mzirudishe mikononi mwenu, labda yuko aliyekosa kwa kupotelewa na amri.#1 Mose 42:27,35. 13Kisha mchukueni naye ndugu yenu, mwondoke kurudi kwake yule mtu! 14Naye Mwenyezi Mungu na awapatie kuhurumiwa usoni pake yule mtu, awafungulie ndugu yenu mwingine, mje naye hata naye Benyamini! Lakini mimi, kama nilivyopotelewa na wana, kama inanipasa, na nipotelewe tena na wana.#1 Mose 42:36.
Yosefu anawapokea ndugu zake vizuri.
15Kisha hao watu wakayachukua hayo matunzo, nazo fedha za mara mbili wakazichukua mikononi mwao, naye Benyamini, wakaondoka kutelemka kwenda Misri. Walipomtokea Yosefu, 16naye Yosefu alipomwona Benyamini kuwa nao, akamwambia mkuu wa nyumba yake: Waingize watu hawa humo nyumbani! Kisha chinja nyama, uiandalie vizuri, kwani watu hawa watakula kwangu saa sita. 17Yule mtu akafanya, kama Yosefu alivyomwagiza, akawaingiza hao watu nyumbani mwa Yosefu. 18Lakini watu hao wakashikwa na woga kwa kuingizwa nyumbani mwake Yosefu, wakasema: Tumeingizwa humu kwa ajili ya hizo fedha zilizorudishwa hapo kwanza katika magunia yetu, apate kutusingizia na kutulipisha yaliyotuangukia, atuchukue sisi pamoja na punda wetu, tuwe watumwa wake.#1 Mose 42:28. 19Kwa hiyo wakamkaribia yule mkuu wa nyumba ya Yosefu, wakasema naye hapo pa kuingia nyumbani, 20wakamwambia: E bwana, tulipotelemka safari ya kwanza kununua ngano, 21nasi tulipofika kambini, tukafungua magunia yetu, tukaona kila mtu fedha zake juu ndani ya gunia lake, nazo hizo fedha zetu zilikuwa zenye kipimo chao sawasawa, kwa hiyo tumezirudisha mikononi mwetu; 22nazo fedha nyingine tumetelemka nazo mikononi mwetu za kununua vilaji; hatumjui aliyeziweka hizo fedha zetu katika magunia yetu. 23Naye akasema: Tulieni tu, msiogope! Mungu wenu na Mungu wa baba yenu aliwapatia kilimbiko katika magunia yenu, fedha zenu zilifika kwangu. Kisha akamfungua Simeoni, akamleta kwao,#1 Mose 42:24. 24akawaingiza nyumbani mwake Yosefu, akawapa maji ya kuiosha miguu yao, nao punda wao akawapata chakula.#1 Mose 18:4. 25Nao wakayatengeneza matunzo yao, mpaka Yosefu akaja saa sita, kwani walisikia, ya kuwa watakula chakula huko.
Yosefu anawaandalia ndugu zake chakula.
26Yosefu alipoingia humo nyumbani, wakampelekea hayo matunzo mikononi mwao nyumbani mwake na kumwangukia hapo chini. 27Akawaamkia kwa upole, akawauliza: Baba yenu mzee, ambaye mliniambia, ya kuwa yuko mzima, na sasa hajambo?#1 Mose 42:13. 28Wakamwambia: Mtumwa wako baba yetu hajambo, yuko mzima bado; kisha wakamwinamia na kumwangukia.#1 Mose 37:7,9. 29Alipoyainua macho yake akamwona ndugu yake Benyamini aliyezaliwa na mama yake, akauliza: Kumbe huyu ni ndugu yenu mdogo, ambaye mliniambia habari zake? Akasema: Mungu na akugawie mema, mwanangu! 30Kisha Yosefu akakimbilia chumba kingine, apate kulia machozi, kwani alichafukwa na moyo kwa kumfurahia nduguye, namo mle chumbani machozi yakamtoka kweli. 31Alipokwisha kuunawa uso wake, akawatokea tena na kutulia kwa kujizuia, akaagiza: Leteni chakula! 32Wakamwandalia yeye peke yake nao ndugu zake peke yao nao Wamisri waliokula naye peke yao, kwani ni mwiko wa Wamisri kula chakula pamoja na Waebureo, huwachukiza.#1 Mose 46:34; 2 Mose 8:26. 33Wakawakalisha mbele yake, kama walivyofuatana: aliyezaliwa wa kwanza hapo palipoupasa ukubwa wake, naye mdogo hapo palipoupasa ujana wake; kwa hiyo hao watu wakastaajabu na kutazamana wao kwa wao. 34Wakawapa vyakula vilivyotoka mezani pake Yosefu, lakini Benyamini akaandaliwa vyakula vilivyovipita vyao wote kwa wingi mara tano. Kisha wakanywa, hata wakachangamshwa pamoja naye.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 43: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: