1 Mose 44
44
Kaka zake Yosefu wanahangaishwa sana.
1Yosefu akamwagiza mkuu wa nyumba yake kwamba: Magunia ya watu hawa yajaze vilaji, kama wanavyoweza kuchukua, nazo fedha za kila mtu ziweke juu ndani ya gunia lake! 2Namo juu ndani ya gunia lake mdogo tia pamoja na fedha zake za ngano kikombe changu, hicho kikombe cha fedha. Akafanya hivyo, kama Yosefu alivyomwagiza. 3Asubuhi kulipopambazuka, wakapewa ruhusa kwenda zao, wao na punda wao. 4Walipokwisha kutoka mjini na kwenda mbali kidogo, ndipo, Yosefu alipomwambia mkuu wa nyumba yake: Ondoka, uwafuate hao watu na kupiga mbio! Utakapowapata waambie: Mbona hayo mema mliyofanyiziwa mnayalipa na kufanya mabaya? 5Kumbe hicho kikombe sicho, bwana wangu alichokinywea? Tena hukitumia cha kuagulia. Haya mliyoyafanya ni mabaya. 6Alipowapata akawaambia maneno yayo hayo. 7Wakamwambia: Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama hayo? Yasiwajie watuma wako maneno kama hayo, wayafanye! 8Tazama! Hizo fedha, tulizoziona juu ndani ya magunia, tumezirudisha kwako toka nchi ya Kanaani. Tutawezaje kuiba fedha au dhahabu nyumbani mwa bwana wako?#1 Mose 43:22. 9Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwao watumwa wako na afe! Nasi tutakaopona tutakuwa watumwa wake bwana wetu. 10Akaitikia kwamba: Basi, na viwe hivyo, kama mlivyosema! Atakayeonekana kuwa nacho, atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine mtakuwa hamna kosa. 11Wakashusha upesi chini kila mtu gunia lake, wakafungua kila mtu gunia lake. 12Naye yule mtu alipotafuta akaanza kwake mkubwa, akamaliza kwake mdogo; ndipo, kikombe kilipooneka katika gunia la Benyamini. 13Ndipo, wote walipozirarua nguo zao, wakawachukuza tena kila mtu punda wake mzigo ake, wakarudi mjini.#1 Mose 37:29.
14Yuda na ndugu zake walipoingia nyumbani mwa Yosefu, naye alikuwa angalimo bado, nao wakamwangukia chini. 15Yosefu akawaambia: Ni tendo gani hilo, mlilolitenda? Hamjui, ya kuwa mtu kama mimi huangua? 16Yuda akajibu: Tumwambie nini bwana wetu? Tusemeje? Tutawezaje kujikania? Mngu anayaumbua maovu, watumwa wako waliyoyafanya; tazama, sisi pamoja naye aliyeonekana kuwa nacho hicho kikombe mkononi mwake tu watumwa wako.#1 Mose 42:21-22; Omb. 1:14. 17Naye akasema: Hili lisinijie, nifanye tendo kama hilo! Yule mtu aliyeoneka kuwa nacho hicho kikombe mkononi mwake yeye tu atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine nendeni na kutengemana kwa baba yenu!
18Ndipo, Yuda alipomkaribia na kumwambia: Tafadhali, bwana wangu, mtumwa wako na aseme neno masikioni pake bwana wangu! Makali yako yasimwakie mtumwa wako! Kwani wewe unalingana na Farao. 19Bwana wangu alipowauliza watumwa wake kwamba: Mna baba au ndugu?#1 Mose 42:7,13; 43:7. 20tukamwambia bwana wangu: Tuna baba, naye ni mzee, naye mtoto wa uzee wake yuko, lakini ndugu yake amekufa, akaachwa yeye peke yake wa mama yake, kwa hiyo baba yake anampenda. 21Ukawaambia watumwa wako: Sharti mmtelemshe, afike kwangu, nipate kumwona kwa macho yangu. 22Nasi tukamwambia bwana wangu: Huyu kijana hataweza kumwacha baba yake; akimwacha baba yake, huyo atakufa. 23Ukawaambia watumwa wako: Ndugu yenu mdogo asipotelemka pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.#1 Mose 42:15; 43:3-5. 24Tulipopanda kwenda kwa mtumwa wako, baba yangu, tukamsimulia hayo maneno ya bwana kidogo! 25Kisha baba yetu alipotuambia: Rudini kutununulia vilaji wangu! 26Tukasema: Hatuwezi kutelemka; lakini ndugu yetu mdogo akienda pamoja nasi, tutatelemka; kwani hatuwezi kuuona uso wake yule mtu, ndugu yetu mdogo asipokuwa nasi. 27Ndipo, mtumwa wako baba yangu alipotuambia: Ninyi mnajua, ya kuwa mke wangu alinizalia wana wawili; 28mmoja alipoondoka kwangu, nikasema: Ameraruliwa na nyama, maana sikumwona tena mpaka sasa.#1 Mose 37:32-33; 1 Mose 42:38. 29Sasa mkimchukua huyu naye na kumtoa kwangu, akipatwwa na kibaya njiani, mtanisukuma mimi mwenye mvi kushuka kuzimuni kwa kuyaona hayo mabaya. 30Kama ningefika kwa mtumwa wako, baba yangu, tusipokuwa naye huyu kijana, ambaye roho ya baba ilifungamana nayo roho yake, 31baba akaona, ya kuwa hayuko, angekufa papo hapo, nasi watumwa wako tungekuwa tunamsukuma mtumwa wako, baba yetu, mwenye mvi kushuka kuzimuni na kusikitika. 32Kwani mimi, mtumwa wako, nimejitoa kwa baba kuwa mdhamini wake huyu kijana, nikamwambia: Nisipomrudisha kwako, nitakuwa nimemkosea baba yangu siku zote.#1 Mose 43:9. 33Sasa mtumwa wako na akae mahali pake huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu, naye huyu kijana na apande na kaka zake kwenda kwao! 34Kwani nitawezaje kupanda kwenda kwa baba yangu, huyu kijana asipokuwa pamoja na mimi? Sitaweza kuyaona hayo mabaya yatakayompata baba yangu.
Iliyochaguliwa sasa
1 Mose 44: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: