Luka 15
15
Kondoo aliyepotea.
1*Watoza kodi na wakosaji wo wote walipokuwa wanamjia, wamsikilize, 2Mafariseo na waandishi wakanung'unika wakisema: Huyu huwapokea wakosaji, ale pamoja nao.#Luk. 5:29-30. 3Ndipo, alipowatolea mfano huu akisema:
(4-7: Mat. 18:12-14.)
4Kwenu yuko mtu mwenye kondoo mia akipoteza mmoja wao, asiyewaacha wale tisini na tisa porini, aende kumtafuta yule aliyepotea, mpaka atakapomwona?#Luk. 19:10; Ez. 34:11,16. 5Naye akimwona anamweka mabegani kwa kufurahi. 6Tena akifika kwao anawaita rafiki zake na majirani zake na kuwaambia: Furahini pamoja nami! Kwani nimemwona kondoo wangu aliyepotea. 7Nawaambiani: Vivyo hivyo mkosaji mmoja anapojuta, kutakuwako huko mbinguni furaha inayoipita ile iliyoko kwa ajili ya waongofu tisini na tisa wasiopaswa na kujuta.
Shilingi iliyopotea
8Au yuko mwanamke mwenye shilingi kumi akipoteza moja, asiyewasha taa na kufagia nyumbani na kuitafuta kwa uangalifu, mpaka atakapoiona? 9Naye akiiona anawaita shoga zake na majirani zake na kusema: Furahini pamoja nami! Kwani nimeiona shilingi yangu, niliyoipoteza. 10Nawaambieni: Vivyo hivyo mkosaji mmoja anapojuta, itakuwako furaha mbele ya malaika za Mungu.*#Ef. 3:10.
Mwana mpotevu.
11*Kisha akasema: Kulikuwa na mtu mwenye wana wawili. 12Aliye mdogo wao akamwambia baba yake: Baba, nipe fungu la mali litakalokuwa langu! Ndipo, alipowagawanyia mali. 13Siku chache zilipopita, mwana mdogo akavikusanya vyote, akajiendea kufika katika nchi ya mbali. Huko akazitapanya mali zake kwa kuzitumia ovyoovyo tu.#Fano. 29:3. 14Alipoziishia zote pia, njaa kubwa ikaiguia nchi ile, naye akaanza kuumia kwa njaa. 15Ndipo, alipokwenda kugandamiana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye akamtuma shambani, achunge nguruwe. 16Akataka sana kulijaza tumbo lake maganda tu, nguruwe waliyokula, lakini hakuna aliyempa.#Fano. 23:21. 17Ndipo, alipojirudia mwenyewe akisema: Vibarua wangapi wako kwa baba yangu wanaoshiba chakula na kusaza, nami hapa ninakufa njaa! 18Nitainuka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu na wewe;#Yer. 3:12-13; Sh. 51:6. 19hainipasi tena kuitwa mwana wako, unitumikishe kuwa kama kibarua wako!
20Kisha akaondoka, akaenda kwa baba yake. Akingali mbali bado, baba yake akamwona, akamwonea uchungu, akapiga mbio, akamkumbatia shingoni, akamnonea. 21Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea Mungu na wewe; hainipasi tena kuitwa mwana wako. 22Lakini baba yake akawaambia watumwa wake: Leteni upesi nguo iliyo nzuri kuliko zote, mmvike! Mtieni hata pete kidoleni na viatu miguuni!#1 Yoh. 3:20. 23Kisha mleteni yule ndama aliyenona, mmchinje, tupate kula na kushangilia! 24Kwani huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana tena. Wakaanza kushangilia.#Ef. 2:1,5; 5:14.
25Lakini mwana wake mkubwa alikuwa shambani; alipokuja na kufika karibu ya mjini akasikia nyimbo na michezo. 26Akaita mtumwa mmoja, akamwuliza: Mambo hayo ya nini? 27Naye akamwambia: Ndugu yako amekuja; ndipo, baba yako alipomchinjia yule ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yuko mzima. 28Akakasirika sana, hakutaka kuingia. Lakini baba yake alipotoka na kumbembeleza,#Luk. 15:2. 29akamjibu baba yake akimwambia: Tazama, miaka hii yote ninakutumikia; tena hakuna agizo lako, nisilolifanya. Nawe hujanipa hata kibuzi, nipate kushangilia na rafiki zangu. 30Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyekula mali zako pamoja na wagoni, umemchinjia yule ndama aliyenona. 31Naye akamwambia: Mwanangu, wewe siku zote uko pamoja nami, nayo yote, niliyo nayo, ni yako. 32Lakini imetupasa kushangilia na kufurahi, kwani huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka. Alikuwa amepotea, naye ameonekana tena.*
Iliyochaguliwa sasa
Luka 15: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: