Luka 20
20
Ubatizo wa Yohana.
(1-8: Mat. 21:23-27; Mar. 11:27-33.)
1Ikawa siku moja, alipofundisha watu hapo Patakatifu na kuipiga hiyo mbiu njema, wakamwinukia watambikaji wakuu na waandishi na wazee, 2wakamwambia wakisema: Utuambie: Hayo unayafanya kwa nguvu gani? au ni nani aliyekupa nguvu hii? 3Akajibu akiwaambia: Hata mimi nitawauliza neno moja, mnijibu: 4Ubatizo wake Yohana ulitoka mbinguni au kwa watu? 5Wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea? 6Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, watu wote watatupiga mawe. Kwani walikuwa wametambua kweli kwamba: Yohana ni mfumbuaji. 7Kwa hiyo wakajibu: Hatujui, ulikotoka. 8Ndipo, Yesu alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.
Wakulima wabaya.
(9-19: Mat. 21:33-46; Mar. 12:1-12.)
9Akaanza kuwatolea watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine kukaa siku nyingi. 10Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, wampe matunda ya mizabibu. Lakini wakulima wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.#2 Mambo 36:15-16. 11Akaongeza kutuma mtumwa mwingine. Naye wale wakampiga na kumtukana, wakamrudisha mikono mitupu. 12Akaongeza kumtuma wa tatu. Naye wale wakamtia vidonda na kumfukuza. 13Ndipo, mwenye mizabibu aliposema: Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu mpendwa, labla huyo watamcha. 14Lakini wakulima walipomwona wakafikiri na kusemezana wao kwa wao: Huyu ndiye kibwana; na tumwue, urithi wake uwe wetu! 15Kwa hiyo wakamsukumasukuma mpaka nje ya mizabibu, wakamwua. Basi, mwenye mizabibu atawafanyia nini? 16Atakuja na kuwangamiza wakulima hao nayo mizabibu atawapa wengine. Wao waliosikia wakasema: Yasiwe hayo! 17Naye akawatazama, akasema: Basi, maana ya neno lililoandikwa ni nini? Hilo la kwamba:
Jiwe, walilolikataa waashi,
hilihili limekuwa jiwe la pembeni?#Sh. 118:22.
18Kila atakayeanguka juu ya jiwe lile atapondeka; naye litakayemwangukia, litambana tikitiki.
Shilingi ya kodi.
19Saa ileile waandishi na watambikaji wakuu wakatafuta kumkamata, lakini waliliogopa lile kundi la watu; kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano lhuo.#Luk. 19:48.
(20-26: Mat. 22:15-22; Mar. 12:13-17.)
20Wakamtunduia, wakatuma wapelelezi, wafanye ujanja wa kuwa kama waongofu, maana wamnase kwa maneno yake, wapate kumpeleka bomani kwenye nguvu ya mtawala nchi.#Luk. 11:54. 21Nao wakamwuliza wakisema: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa unasema ya kweli na kuyafundisha, hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli. 22Sisi tuko na ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi, au haiko? 23Kwa kuujua werevu wao mbaya, akawaambia: 24Nionyesheni shilingi! Ina chapa na maandiko ya nani? Nao wakasema: Yake Kaisari. 25Ndipo, alipowaambia: Basi, yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu! 26Hivyo hawakuweza kumnasa kwa maneno yake mbele za watu, wakamstaajabu, alivyojibu, wakanyamaza.
Kufufuka.
(27-40: Mat. 22:23-33,46; Mar. 12:18-27,34.)
27Kulikuwa na Masadukeo wanaobisha kwamba: Hakuna ufufuko; wakamjia, wakamwuliza wakisema: 28Mfunzi, Mose alitundikia: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyekuwa na mkewe pasipo kuwa na mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.#5 Mose 25:5-6. 29Kulikuwa na waume saba walio ndugu. 30Wa kwanza akaoa mke, akafa pasipo kuwa na mwana. 31Naye wa pili, kisha wa tatu akamchukua yule mwanamke; vivi hivi hata wale saba, hawakuacha wana walipokufa. 32Mwisho akafa naye mwanamke. 33Basi, katika ufuko huyo mwanamke atakuwa mke wa yupi wa hao? Kwani wote saba walikuwa naye yule mwanamke. 34Yesu akawaambia: Wana wa dunia hii huoa, tena huolewa. 35Lakini wale watakaopewa kuifikia dunia ile na kufufuliwa katika wafu hawataoa, wala hawataolewa. 36Kwani hawataweza kufa tena, maana watafanana na malaika, watakuwa wana wa Mungu kwa hivyo, walivyofufuka.#1 Yoh. 3:1-2. 37Lakini kwa ajili ya wafu, kwamba wafufuliwa, hata Mose alivifumbua kidogo hapo kichakani alipomwita Bwana: Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.#2 Mose 3:2,6. 38Lakini Mungu siye wa wafu, la wao walio hai; kwani kwake wote huishi. 39Kulikuwa na waandishi waliojibu wakisema: Mfunzi, umesema vema. 40Kwani hawakujipa moyo tena kumwuliza neno.
Mwana wa Dawidi.
(41-44: Mat. 22:41-45; Mar. 12:35-37.)
41Kisha akawaambia: Husemaje, ya kuwa Kristo ni mwana wa Dawidi? 42Kwani Dawidi mwenyewe asema katika kitabu cha Mashangilio:
Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu,#Sh. 110:1.
43mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
44Basi, Dawidi akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake?
Kujilinda kwa ajili ya waandishi.
(45-47: Mat. 23:1, 5-7,14; Mar. 12:38-40.)
45Akawaambia wanafunzi, watu wote waliposikia:#Luk. 11:43. 46Jilindeni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni! Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu. 47Huzila nyumba za wajane, wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.
Iliyochaguliwa sasa
Luka 20: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: