Luka 21
21
Hela la mjane.
(1-4: Mar. 12:41-44.)
1Alipoinua macho akaona, wenye mali walivyotia sadaka zao katika sanduku ya vipaji. 2Akaona hata mwanamke mjane aliyekuwa mkiwa, alivyotia mle visenti viwili. 3Ndipo, aliposema: Kweli nawaambiani: Huyu mjane mkiwa ametia mengi kuliko wote. 4Kwani hao wote walitoa mali katika mali zao nyingi, wakazitia penye sadaka, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vilivyomlisha.
Mambo yatakayokuja.
(5-24: Mat. 24:1-21; Mar. 13:1-19.)
5Wengine waliposema, Patakatifu palivyokuwa pamepambwa na mawe mazuri na mapambo mengine, ndipo, aliposema: 6Je? Mwayatazama haya? Siku zitakuja, ambapo halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini. 7Wakamwuliza wakisema: Mfunzi, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yatakapotimia? 8Naye akasema: Angalieni, msipotezwe! Kwani wengi watakuja kwa Jina langu na kusema: Mimi ndiye, nazo siku zimekwisha kufika. Msiwafuate hao! 9Nanyi mtakaposikia vita na mainukiano, msitukutike! Kwani hayo sharti yawepo kwanza; lakini mwisho hauji upesi. 10Ndipo alipowaambia: Watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme. 11Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko makuu, pengine na kipindupindu, pengine na njaa. Hata vielekezo vikubwa vitatokea mbinguni vya kuogofya. 12Lakini hayo yote yatakapokuwa hayajatimia bado, watawanyoshea mikono, wawakamate na kuwakimbiza, wawapeleke nyumbani mwa kuombea namo mabomani, wawaweke mbele yao wafalme na mabwana wakubwa kwa ajili ya Jina langu.#Luk. 12:11. 13Hayo yatawapata ninyi, mje kunishuhudia kwao.#Mat. 10:18. 14Jueni, nguvu imo mioyoni mwenu, msianze kuyahangaikia maneno ya kujikania!#Mat. 10:19. 15Kwani mimi nitawapa vinywani maneno yenye werevu wa kweli; nao wabishi wenu wote hawataweza kuyabisha wala kuyakana.#Tume. 6:10. 16Nanyi mtatolewa na wazazi na ndugu na wenzenu wa ukoo na rafiki; wengine wenu watawaua, 17nanyi mtakuwa mmechukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu.#Mat. 10:21-22. 18Lakini hata unywele mmoja hautawapotelea vichwani,#Luk. 12:7; Mat. 10:29-30. 19ila kwa kuvumilia mtazikomboa roho zenu.
20Lakini hapo mtakapoona, mji wa Yerusalemu ukizungukwa na vikosi, ndipo mjue, ya kuwa kuangamizwa kwake kumetimia.#2 Mambo 15:7; Ebr. 10:36. 21Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani! Nao watakaokuwamo mle mjini watoke! Nao watakaokuwako shambani wasiuingie tena! 22Kwani siku hizo zitakuwa za malipizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.#5 Mose 32:35; Yer. 5:29. 23Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile. Kwani itakuwa kondo kubwa katika nchi, makali yatakapowatokea watu wa kabila hili: 24wengine wataanguka kwa ukali wa panga, wengine watatekwa na kutawanyishwa kwenye mataifa yote. Namo Yerusalemu mtakanyagwa na wamizimu, mpaka siku za wamizimu zitakapotimizwa.#Sh. 79; Rom. 11:25; Ufu. 11:2.
(25-28: Mat. 24:29-30; Mar. 13:24-26.)
25*Kutakuwa na vielekezo vya jua na vya mwezi na vya nyota. Huku nchini watu wa mataifa yote watapotelewa na mioyo wasipojua maana, mawimbi ya bahari yatakapokaza kuvuma na kutukutika. 26Ndipo, watu watakapozimia kwa woga na kwa kuyangoja mambo yatakayopajia pote, wanapokaa, kwani hata nguvu za mbingu zitatukutishwa. 27Hapo ndipo, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja katika wingi mwenye nguvu na utukufu mwingi.#Dan. 7:13. 28Lakini hayo yatakapoanza kuwapo, myaelekeze macho yenu mbinguni na kuviinua vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu utakuwa uko karibu!#Dan. 4:4-5.
(29-33: Mat. 24:32-35; Mar. 13:28-31.)
29Kisha akawaambia mfano: Utazameni mkuyu na miti yote! 30Mnapoiona, ikichipua, mnatambua wenyewe, ya kuwa siku za vuli zimekwisha kuwa karibu. 31Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo, yakiwapo, tambueni, ya kuwa ufalme wa Mungu umewafikia karibu! 32Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo yote. 33Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.#Luk. 16:17. 34Lakini jilindeni, ulafi na ulevi na masumbuko ya nchini yasiwalemee mioyoni, siku ile isiwajie, msipoingoja!#Mar. 4:19. 35Kwani kama mtego unavyonasa, itawajia wote po pote, wanapokaa nchini.#1 Tes. 5:3. 36Kesheni siku zote na kuomba, mpate nguvu za kuyakimbia hayo yote, yatakayokuwapo, msimamishwe mbele ya Mwana wa mtu!*#Mar. 13:33.
37Akawa kila siku akifundisha Patakatifu, lakini usiku hutoka na kulala kwenye mlima unaoitwa Wa Michekele. 38Nao watu wote walikuwa wakimwendea asubuhi pale Patakatifu, wamsikilize.
Iliyochaguliwa sasa
Luka 21: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: