Kutoka Utangulizi
Utangulizi
Kitabu cha Kutoka kinazungumzia mambo muhimu yanayohusu kuinuka kwa Israeli kama taifa. Uongozi mzuri wa Musa unaelezewa kuanzia alivyokubali wito wa Mwenyezi Mungu kurudi Misri ili kuwaongoza watu wa Mungu kwa uhuru. Mwenyezi Mungu alituma mapigo kumi ya kuangamiza Misri kwa sababu Farao alikataa kutii amri yake. Adhimisho la Pasaka lilianzishwa wakati wa pigo la mwisho, na likawa ukumbusho wa ukombozi wa Mwenyezi Mungu kwa wakati wote kwa Israeli. Wana wa Israeli walivuka bahari na kufika Mlima Sinai ambapo Mwenyezi Mungu aliwapa amri kumi, na mpango wa Maskani ya Mungu, na kufanya Agano lake upya na taifa.
Wazo Kuu
Nguvu za Mwenyezi Mungu juu ya uovu zinaonyeshwa kwa wazi wakati Mungu anawashinda maadui wa watu wake kwa kuwaokoa kutoka utumwani. Lakini Mwenyezi Mungu anatarajia nasi tumwamini na kumtii. Kuabudu katika Maskani ya Mungu na kutii sheria vilikuwa vipengele viwili vya kutii kwa Israeli. Kondoo wa Pasaka anaonekana katika Injili kama taswira ya Al-Masihi, aliye Mwana-Kondoo wa Mungu (1 Wakorintho 5:7).
Mwandishi
Musa.
Tarehe
Mwaka wa 1420 au 1220 KK.
Mgawanyo
Utumwa wa Israeli kule Misri (1:1-22)
Maisha ya mwanzo ya Musa (2:1–7:7)
Mapigo, Pasaka, na kutoka kwa Waisraeli kule Misri (7:8–15:21)
Safari ya kwenda Sinai, na kupewa Torati (15:22–24:18)
Maagizo ya Maskani ya Mungu (25:1–31:18)
Dhambi ya Israeli na kurejezwa kwao (32:1–35:3)
Kujengwa kwa Maskani ya Mungu (35:4–40:38).
Iliyochaguliwa sasa
Kutoka Utangulizi: NMM
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018 by Biblica, Inc.
Used with permission.
All rights reserved worldwide.