Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wafalme UTANGULIZI

UTANGULIZI
Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya kwanza ya kitabu kimoja ambacho kiligawanywa kuwa viwili kwa sababu kilikuwa kirefu mno kuweza kuwa katika msokoto mmoja. Vitabu hivyo pamoja vinaendelea na historia ya Waisraeli pale Kitabu cha Pili cha Samueli kilipoachia. Lakini vitabu hivyo vinaeleza historia hiyo kwa namna ya pekee.
Kitabu cha kwanza cha Wafalme kinaanza kwa kueleza mambo ya mwisho ya Daudi na kuchukua madaraka ya ufalme kwa upande wa Solomoni. Kisha tunaelezwa visa mbalimbali vya utawala wa Solomoni, kilele cha habari hizo kikiwa ujenzi na kuwekwa wakfu kwa hekalu. Kisha tunaelezwa jinsi utawala huo mkubwa wa Daudi ulivyogawanyika na kuwa sehemu mbili zilizotengana: Ufalme wa kaskazini, yaani Israeli, na ufalme wa kusini, yaani Yuda.
Vitabu hivyo vya Wafalme vinatupatia visa mbalimbali vya wafalme wa Waisraeli kadhalika na mambo mengine. Walakini visa hivyo havitolewi tu kama historia. Vitabu hivyo au habari hizo zote aghalabu zinaonesha namna ilivyo muhimu kabisa kwa mfalme kuwa mwaminifu kwa Mungu. Uaminifu wa namna hiyo huleta fanaka na ustawi kwa taifa lote, hali kuabudu miungu mingine, jambo ambalo mara kwa mara linaelezwa hasa katika vitabu vya manabii kama kufanya uzinzi, ukosefu wa utii kwa Mungu, n.k., husababisha adhabu na maangamizi. Manabii kadha wa kadha waliwakumbusha wafalme hao juu ya jambo hilo. Nabii mmojawapo mashuhuri aliyekuwa na jukumu hilo ni Elia (sura 17:1–19:21).
Kitabu hiki chaweza kugawanyika katika sehemu mbili kuu:
Sura 1-11: Utawala wa Solomoni.
Sura 12-22: Historia za tawala za Yuda na Israeli karne ya kwanza baada ya kutengana mpaka wakati wa mfalme Ahazi.

Iliyochaguliwa sasa

1 Wafalme UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia