Amosi 9:11-15
Amosi 9:11-15 BHN
“Siku yaja nitakapoisimika nyumba ya Daudi iliyoanguka; nitazitengeneza kuta zake, na kusimika upya magofu yake. Nitaijenga upya kama ilivyokuwa hapo zamani. Nao Waisraeli watamiliki mabaki ya Edomu na mataifa yote yaliyokuwa yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema, na nitafanya hivyo. “Wakati waja kwa hakika, ambapo mara baada ya kulima mavuno yatakuwa tayari kuvunwa; mara baada ya kupanda mizabibu utafuata wakati wa kuvuna zabibu. Milima itabubujika divai mpya, navyo vilima vitatiririka divai. Nitarekebisha hali ya watu wangu Waisraeli. Watajenga miji yao iliyoharibiwa na kuishi humo; watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima mashamba na kula mazao yake. Nitawasimika katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena kutoka katika nchi niliyowapa. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”