Mhubiri 1:13-18
Mhubiri 1:13-18 BHN
Nilipania kuchunguza na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachotukia duniani. Hiyo ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu. Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: Ni sawa na kufukuza upepo! Kilichopindika hakiwezi kunyoshwa, kisichokuwapo hakiwezi kuhesabiwa. Basi, nikatafakari nikisema, “Nimejipatia hekima nyingi zaidi kupita wote waliopata kutawala Yerusalemu kabla yangu. Naam, nina uzoefu wa hekima na maarifa.” Nilipania kubainisha kati ya hekima, wazimu na upumbavu. Lakini niligundua kwamba kufanya hivyo ni sawa na kufukuza upepo. Maana katika kuwa na hekima nyingi mna wasiwasi; na aongezaye maarifa zaidi huongeza huzuni zaidi.