Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 13:12-16

Hosea 13:12-16 BHN

“Uovu wa Efraimu uko umeandikwa, dhambi yake imehifadhiwa ghalani. Maumivu kama ya kujifungua mtoto yanamfikia. Lakini yeye ni mtoto mpumbavu; wakati ufikapo wa kuzaliwa yeye hukataa kutoka tumboni kwa mama! Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma! “Hata kama Efraimu atastawi kama nyasi, mimi Mwenyezi-Mungu nitavumisha upepo wa mashariki, upepo utakaozuka huko jangwani, navyo visima vyake vitakwisha maji, chemchemi zake zitakauka. Hazina zake zote za thamani zitanyakuliwa.” Watu wa Samaria wataadhibiwa kwa kosa lao. Kwa sababu wamemwasi Mungu wao. Watauawa kwa upanga, vitoto vyao vitapondwapondwa, na kina mama wajawazito watatumbuliwa.

Soma Hosea 13