Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 18

18
Mungu ataiadhibu Kushi
1Ole, wake nchi iliyojaa mvumo wa mabawa,
nchi iliyoko ngambo ya mito ya Kushi!#18:1 Kushi: Nubia au Ethiopia.
2Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili,
wamepanda mashua za mafunjo.
Nendeni, enyi wajumbe wepesi,
kwa taifa kubwa na hodari,
la watu warefu na wa ngozi laini.
Watu hao wanaoogopwa kila mahali
na nchi yao imegawanywa na mito.
3Enyi wakazi wote ulimwenguni,
nanyi mkaao duniani!
Ishara itakapotolewa mlimani, tazameni!
Tarumbeta itakapopigwa, sikilizeni.
4Maana, Mwenyezi-Mungu ameniambia hivi:
“Toka makao yangu juu nitatazama yanayotukia,
nimetulia kama joto katika mwanga wa jua,
kama wingu la umande wakati wa mavuno.
5Maana, kabla ya mavuno,
wakati wa kuchanua umekwisha,
maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu,
Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea,
na kuyakwanyua matawi yanayotanda.
6Yote yataachiwa ndege milimani,
na wanyama wengine wa porini.
Ndege walao nyama watakaa humo
wakati wa majira ya kiangazi,
na wanyama wa porini watafanya makao humo
wakati wa majira ya baridi.”
7Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.

Iliyochaguliwa sasa

Isaya 18: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia