Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 10

10
Kauli ya mwisho ya Yobu
1“Nayachukia maisha yangu!
Malalamiko yangu nitayasema bila kizuizi.
Nitasema kwa uchungu wa moyo wangu.
2Nitamwambia Mungu: Usinihukumu.
Nijulishe kisa cha kupingana nami.
3Je, ni sawa kwako kunionea,
kuidharau kazi ya mikono yako
na kuipendelea mipango ya waovu?
4Je, una macho kama ya binadamu?
Je, waona kama binadamu aonavyo?
5Je, siku zako ni kama za binadamu?
Au miaka yako kama ya binadamu,
6hata uuchunguze uovu wangu,
na kuitafuta dhambi yangu?
7 # Taz Hek 16:15 Wewe wajua kwamba mimi sina hatia,
na hakuna wa kuniokoa mikononi mwako.
8Mikono yako iliniunda na kuniumba,
lakini sasa wageuka kuniangamiza.
9Kumbuka kwamba uliniumba kwa udongo.
Je, utanirudisha tena mavumbini?
10 # Taz Hek 7:1-7 Je, si wewe uliyenimimina kama maziwa,
na kunigandisha kama jibini?
11Uliuumba mwili wangu kwa mifupa na mishipa,
ukaifunika mifupa yangu kwa nyama na ngozi.
12Umenijalia uhai na fadhili,
uangalifu wako umeisalimisha nafsi yangu.
13Hata hivyo mambo haya uliyaficha moyoni.
Lakini najua kuwa hiyo ilikuwa nia yako.
14Ulikuwa unangojea uone kama nitatenda dhambi,
ili ukatae kunisamehe uovu wangu.
15Kama mimi ni mwovu, ole wangu!
Kama mimi ni mwadilifu, siwezi kujisifu;
kwani nimejaa fedheha, nikiyatazama mateso yangu.
16Nikiinua kichwa tu waniwinda kama simba
na kuniponda tena kwa maajabu yako.
17Kila mara unao ushahidi dhidi yangu;
waiongeza hasira yako dhidi yangu,
waniletea maadui wapya wanishambulie.
18“Ee Mungu, kwa nini ulinitoa tumboni mwa mama?
Afadhali ningekufa kabla ya watu kuniona.
19Ningepelekwa moja kwa moja kaburini,
nikawa kama mtu asiyepata kuwako.
20Je, siku za maisha yangu si chache?
Niachie nipate faraja kidogo,
21kabla ya kwenda huko ambako sitarudi,
huko kwenye nchi ya huzuni na giza nene;
22nchi ya huzuni na fujo,
ambako mwanga wake ni kama giza.”

Iliyochaguliwa sasa

Yobu 10: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia