Luka 22:14-20
Luka 22:14-20 BHN
Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake. Akawaambia, “Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika ufalme wa Mungu.” Kisha akatwaa kikombe cha divai, akashukuru, akasema, “Pokeeni, mgawane. Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.” Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.” Akafanya vivyo hivyo na kikombe cha divai baada ya chakula, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu.