Mathayo 1:1-6
Mathayo 1:1-6 BHN
Yesu Kristo alikuwa wa ukoo wa Daudi, wa ukoo wa Abrahamu. Hii ndiyo orodha ya ukoo wake: Abrahamu alimzaa Isaka, Isaka alimzaa Yakobo, Yakobo alimzaa Yuda na ndugu zake, Yuda alimzaa Peresi na Zera (mama yao alikuwa Tamari), Peresi alimzaa Hesroni, Hesroni alimzaa Rami, Rami alimzaa Aminadabu, Aminadabu alimzaa Nashoni, Nashoni alimzaa Salmoni, Salmoni alimzaa Boazi (mama yake Boazi alikuwa Rahabu) Boazi na Ruthu walikuwa wazazi wa Obedi, Obedi alimzaa Yese, naye Yese alimzaa Mfalme Daudi. Daudi alimzaa Solomoni (mama yake Solomoni alikuwa Bath-Sheba mke wa Uria).