Filemoni UTANGULIZI
UTANGULIZI
Miongoni mwa barua zote za Agano Jipya, barua hii ya Paulo kwa rafiki yake Filemoni ni ya pekee. Kati ya barua zote za Paulo barua hii ndiyo fupi zaidi kuliko zote, tena ni barua ya binafsi. Katika aya ya 9 inaonekana kuwa Paulo sasa ni mzee. Tena, tofauti na barua nyingine za Paulo ambazo kwa wingi alimpa mtu aandike yale aliyosema na mara nyingine akaweka sahihi yake mwenyewe mwishoni, barua hii aliiandika yeye mwenyewe (aya ya 19).
Anayeandikiwa ni Filemoni, mtu mashuhuri aliyeongokea imani ya Kikristo. Alikuwa na mtumwa mmoja jina lake Onesimo.
Sababu za barua hii ni wazi: Onesimo alikuwa amemtoroka bwana wake, na habari hizo zikamfikia Paulo. Paulo aliamua kumrudisha kwa mwenyewe, kwa hiyo akaandika barua hii, akamwomba Filemoni ampokee sio kama mtumwa tena, bali kama ndugu katika Kristo. Paulo hatuambii kwa nini Onesimo alimtoroka Filemoni (rejea aya 18).
Kwanza Paulo anamsalimu Filemoni na wale anaokaa nao (1-3). Kisha anamshukuru Mungu kwa ajili ya imani na bidii ya Filemoni (4-7). Halafu anamweleza Filemoni wasiwasi wake kumhusu Onesimo na kumwomba ampokee tena, kana kwamba anampokea Paulo mwenyewe (aya 12,17); tena ampokee sio kama mtumwa, bali kama “ndugu yetu mpenzikama ndugu katika Bwana” (aya 15-16).
Iliyochaguliwa sasa
Filemoni UTANGULIZI: BHN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.