Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 26:1-12

Methali 26:1-12 BHN

Heshima apewayo mpumbavu haimfai; ni kama theluji ya kiangazi, au mvua ya wakati wa mavuno. Kama shomoro au mbayuwayu wasiotua, kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Usimjibu mpumbavu kipumbavu, usije ukafanana naye. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.

Soma Methali 26

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Methali 26:1-12