Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 16

16
Kuomba usalama
(Utenzi wa Daudi)
1Unilinde ee Mungu;
maana kwako nakimbilia usalama.
2Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu;
sina jema lolote ila wewe.”
3Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini,
kukaa nao ndiyo furaha yangu.#16:3 Ni bora … yangu: Au Na kuhusu miungu ya uongo humu nchini, mimi nilidhania kuwa ina nguvu.
4Lakini wanaoabudu miungu mingine,#16:4 Lakini … mengi: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
watapata mateso mengi.
Tambiko ya damu sitaitolea kamwe,
na majina ya miungu hiyo sitayataja.
5Wewe ee Mwenyezi-Mungu ndiwe riziki yangu kuu,
majaliwa yangu yamo mikononi mwako.
6Umenipimia sehemu nzuri sana;
naam, urithi wangu ni wa kupendeza.
7Namsifu Mwenyezi-Mungu kwa kuniongoza,
usiku dhamiri yangu yanionya.
8 # Taz Mate 2:25-28 Namweka Mwenyezi-Mungu mbele yangu daima;
yuko pamoja nami, wala sitatikisika.
9Kwa hiyo nitafurahi kwa moyo wote na kushangilia,
nami nitakaa salama salimini.
10 # Taz Mate 13:35 Naam wewe hutaiacha nafsi yangu kuzimu,
hutaniacha mimi mwaminifu wako nipate kuoza.
11Wanionesha njia ya kufikia uhai;
kuwako kwako kwanijaza furaha kamili,
katika mkono wako wa nguvu mna mema ya milele.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 16: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia