Zaburi 2:7-12
Zaburi 2:7-12 BHN
Mfalme asema: “Nitatangaza azimio la Mwenyezi-Mungu. Mungu aliniambia: ‘Wewe ni mwanangu, mimi leo nimekuwa baba yako. Niombe nami nitakupa mataifa yawe urithi wako, na dunia nzima kuwa mali yako. Utawaponda kwa fimbo ya chuma; utawavunja kama chungu cha mfinyanzi!’” Sasa enyi wafalme, tumieni busara; sikilizeni onyo hili, enyi watawala wa dunia. Mtumikieni Mwenyezi-Mungu kwa uchaji; msujudieni na kutetemeka; asije akakasirika, mkaangamia ghafla; kwani hasira yake huwaka haraka. Heri yao wote wanaokimbilia usalama kwake!


