Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 28:1-9

Zaburi 28:1-9 BHN

Nakulilia, ee Mwenyezi-Mungu! Ewe mwamba wa usalama wangu usiniwie kama kiziwi, la sivyo kama usiponisikiliza, nitakuwa kama wale washukao shimoni kwa wafu. Sikiliza sauti ya ombi langu, ninapokulilia unisaidie, ninapoinua mikono yangu kuelekea maskani yako takatifu. Usinipatilize pamoja na watu wabaya, pamoja na watu watendao maovu: Watu wasemao na wenzao maneno ya amani, kumbe wamejaa uhasama moyoni. Uwaadhibu kadiri ya matendo yao, kufuatana na maovu waliyotenda. Waadhibu kadiri ya matendo yao wenyewe; uwatendee yale wanayostahili. Hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu; hawatambui mambo aliyoyafanya. Kwa sababu hiyo atawabomoa, wala hatawajenga tena upya. Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, maana amesikiliza ombi langu. Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu na ngao yangu; tegemeo la moyo wangu limo kwake. Amenisaidia nami nikashangilia kwa moyo; kwa wimbo wangu ninamshukuru. Mwenyezi-Mungu ni nguvu ya watu wake; yeye ni kimbilio la wokovu kwa mfalme wake mteule. Ee Mungu, uwaokoe watu wako; uwabariki watu hao walio mali yako. Uwe mchungaji wao na kuwategemeza milele.

Soma Zaburi 28